Mtihani wa Kiswahili 1 Kidato cha Sita 2024 NECTA
Muda: Saa 3 Sehemu A (Alama 40) Jibu maswali yote katika sehemu hii. 1. soma shairi lifuatalo kwa makini kisha jibu maswali yanayofuata: Majira pia Nipashe , taarifa nazitoa Na redio niwabishe, kama ikiwafikia Majirani niwapashe, jambo nilokusudia Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni. Ndege nawaelezea, tabia yake murua kucheka yake tabia, kununa hakuzoea Wageni wakiingia, fadhila huwatendea Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni. Tabia za firauni, hana ninawaapia Na kuranda mitaani, si yake hiyo tabia Marafiki wa Kihuni, hapendi kuwasikia Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni. Kisa niwaelezeni, tunduni nikamtoa Msusa nambari wani, kisa si kisa alia Hilo kosa namba wani, huzuni imenitia Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni. Lingine lilochangia, tunduni nikamtoa Kosa sugu nadhania, sijui kama sawia Kufuga ndege Songea, sijui kama sawia Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni. Mara aliposikia, mwingine nimechukua Tundu akalibomoa, porini akakimbia Goti nikampigia, katu kanikatalia Ndege ni...