Posts

Uhakiki wa Tamthiliya ya Shujaa Mirambo

Image
Wasiliana na Mwalimu ili Kujiunga Darasa la Uhakiki wa Vitabu vyote vya Fasihi Mtaala Mpya kwa Kugusa Hapa Mwandishi: Emmanuel Mbogo Mwaka: 2021 Utangulizi Tulikaa kwa utulivu ndani ya ukumbi wa TASUBA , tulitazama mbele kwa utulivu tukiwatazama waigizaji wakiigiza tamthiliya maarufu iliyoandikwa na Profesa Aldin Mutembei, ikaporwa na kuuziwa Medical Aid Foundation, tamthiliya yenyewe iliitwa Kilio Chetu. Pembeni yangu alikaa Emmanuel Mbogo ambaye ndiye aliyewaleta waigizaji wale na aliwaongoza katika uigizaji wao. Mbogo alivalia suruali pana ya jinzi, hata shati lake nalo lilikuwa pana. Kama ungetaka kuyafahamu mapana na marefu, basi ungemtazama Mbogo ungeyaona siku hiyo. Hatukuongea neno, tulitazama onyesho lile bila ya sisi kutazamana. Sikuwa na jambo la kuongea na Emmanuel Mbogo , wakati elimu ilitufanya Mimi Mwalimu Makoba, Mugyabuso Mulokozi, Wole Soyinka na wasomi wengi wanaofikiri sawasawa tuufahamu ukweli kwamba dini za kigeni zilitumika kufuta utambulisho, utamaduni, na mfum...

Uhakiki wa Tamthiliya ya Mukwava wa Uhehe

Image
Wasiliana na Mwalimu ili Kujiunga Darasa la Uhakiki wa Vitabu vyote vya Fasihi Mtaala Mpya kwa Kugusa Hapa Mwandishi: Mugyabuso Mulokozi Mwaka: 1979 Mhakiki: Mwalimu Makoba Utangulizi Nikiwa chuo kikuu cha Dar es Salaam , katika ofisi za TATAKI, mwalimu wangu, Profesa Mulokozi alinipita akiwa amebeba vitabu na nyaraka nyingi, mbele kidogo alidondosha vitabu viwili, nikasogea ili nimsaidie kuviokota, lakini nilichelewa, aliviokota haraka kisha akaendelea na safari yake. Alitembea kwa kasi iliyomshangaza kila aliyemtazama. Haikuwa kawaida ya Mulokozi kubebelea mibuku mingi namna ile, wazo likanijia, pengine anakwenda Botswana! Agosti mwaka 2015, alialikwa Botswana kuhudhuria utetezi wa tasnifu ya PhD ya mwanafunzi wa Kezilahabi. Kezilahabi alimpokea vizuri na alikaa Gaborone kwa takribani wiki moja. Mulokozi mwenyewe alikiri wazi kuwa, kukaa na Kezilahabi ulikuwa ni wakati wa furaha na burudani sana kwake. Pia Kezilahabi alitamani sana wabadilishane nafasi, Mulokozi aende Botswana kwa m...