MSIMLAUMU ANTHONY JOSHUA, AMEFANYA KAZI NILIYOMTUMA
Haina
ubishi tena kuwa Anthony Joshua ndiye mfalme wa ndondi katika zama zetu. Laiti kama
angeishi katika zama za akina Mohammed Alli, George Foreman, na Joe Frazier
historia ingebadilika kidogo. Kizazi cha akina Tyson, Evander na Lenox Lewis
hakimuwezi, mwakilishi wao Klitchko kapigwa vilivyo.
Pambano
lake la leo, limefunika pambano la wale vijana wa uzito wa manyoya, Mayweather
na mwenzake Pacquiao… ngumi zimepigwa mpaka kivumbi kikatimuka.
Kabla
pambano halijaanza, nilipata kumtumia ujumbe kijana wangu Anthony Joshua
uliosomeka, “its not over untill its over”, Joshua hakusita kuujibu kwa kusema,
“Next Stop The Ring.” Kisha akazima data.
Pambano
la Klitchko na Joshua lilipoanza, round ya kwanza mpaka ya tano, Joshua
alishambulia sana kwa mapigo yote ya kifundi. Watu walimshangilia kama kawaida,
huku mimi nikitafuta namna nzuri ya yeye kushinda.
Ilipofika
Round ya sita, Joshua alionekana kuchoka kidogo hii ni kwa sababu kwa round
tano mfululizo alikuwa akirusha makonde, basi mpinzani wake kutoka urusi,
akaitumia nafasi hiyo. Klitchko alirusha jeb kali, ikampata Anthony, wakati
bado hajatafakari Klichko akaongeza right hook kali sana ambayo ilimdondosha
chini Anthony. Ukumbi wote ukakaa kimya, watu wakajua tayari Klitchko kashinda,
naye Klitchko, akajiandaa kushangilia ushindi. Wakati Anthony akiwa chini
akiugulia maumivu ya ngumi mbili nzito, ndipo akayakumbuka maneno yangu
niliyomwambia kabla ya pambano, “Its not over untill its over.” Kijana akajikaza
kiume, akainuka ili aendelee kupambana, akafuta jasho katika bega lake la kulia
ambalo amelichora ramani ya Afrika. Akaanza tena kurusha ngumi.
Katika
raundi ya kumi na moja, Joshua aliamua kumaliza mchezo, alirusha jeb kali,
ikaupiga uso wa Klitchko, akapiga jeb tena, mara right hook, jeb, right hook,
jeb, upper cut, jeb, right… oooh salalee Klitchko huyo, kadondoka chini. Lakini
Klitchko naye si wa mchezo, akajizoazoa na kusimama. Khe! ni kama aliuchokonoa
mzinga wa nyuki… alipokea ngumi kali mfululizo zilizomfanya amung’unyemung’unye
maneno. Mara huyoo chali kifo cha mende. Joshua kamaliza kazi niliyomtuma. USHINDI!
#Makoba