MWIZI WA SIMU YANGU
Mwizi! Alipokonya simu yangu, kisha akakimbia... Nami nikaanza
kumkimbiza. Tukakimbizana.
Alipofika mbele kidogo akakunja kona, NIKAKUNJA NAYE. Haikuchukua
muda akazama katika kichaka, NIKAZAMA NAYE. Akaibukia katika shamba la mpemba,
NIKAIBUKA NAYE. Akaamua kunyoosha njia, NIKANYOOKA NAYE.
Alipoona hali imekuwa ngumu, akachomoa kisu kidogo cha
kuchinjia kuku ili anitishe. Mimi nikachomoa panga kubwa la kuchinjia ng'ombe ili
aniogope! Akashusha chini kisu chake, nikashusha chini panga langu, kisha nikamuuliza.
"Utarudisha simu yangu au tuendelee kukimbizana kama wapenzi wapya wa kihindi?"
Hakuwa na maneno mengi, akanipa simu yangu, nikaipokea nikitabasamu. Mwizi aka'jamba'
kwa mshangao!
NIKAJAMBA NAYE.
#Makoba.