TATHMINI YA WAGOMBEA NAFASI YA URAIS-DARUSO (UDSM)
Anaandika Makoba Daud
Japokuwa Wagombea wote
wamepitishwa na kamati ya wapiga ramli, tena wagombea hawana mvuto kuanzia sera
mpaka majina yao, hatuwezi kususa kabisa kuutazama uchaguzi na mwenendo wa
kampeni zao.
RICHARD
Anatilia mkazo suala la kusoma
mapato na matumizi ya DARUSO.
Pia anahoji uhalali wa kulipa
nauli katika mabasi ya CRDB.
Amekopa hoja ya Charles William ya
kuwalipa posho ma CR.
CHANGAMOTO
Wakati wa uzinduzi wa kampeni,
hakupata kusikilizwa na watu wengi japo alijieleza vizuri. Kuna mpinzani wake
alicheza mchezo mchafu wa kuwatoa watu nje ili kupunguza upinzani.
Pia Hatajwi sana katika mitandao
ya kijamii.
*Siku hii ya mwisho, anaonekana kuanza
kukubalika na watu wengi. Hivyo ashone suti nyeusi, huenda akawa raisi.
EMANNUEL
Anataka kuirudisha DARUSO kwa wana
DARUSO. Anadai yeye sio kiongozi wa kujikombakomba na kujipendekeza.
Amekopa hoja ya Shamira Mshangama
inayotaka Dean afanye kazi ya kushauri wanafunzi na si vinginevyo.
CHANGAMOTO
Watu hawana imani naye kwa sababu
ni kada wa waziwazi wa CCM, tena aliyegombea cheo kidogo akashindwa.
Pia, Kamati yake ya kampeni
inalaumiwa kuendesha sera za ukoleji.
*Hata hivyo anazungumzwa sana
katika mitandao ya kijamii. Hii ni faida kwani watu wengi watamfahamu. Bila
shaka yoyote, ang'arishe viatu vyake, huenda akawa rais.
JEREMIAH
Anasema, serikali yake itawapa
wanafunzi uhuru wa kuhoji mambo mbalimbali bila kuingiliwa wala kufukuzwa.
Anasisitiza kwamba, endapo atashindwa kutimiza yale aliyowaahidi wanaDARUSO,
yuko tayari kuondolewa.
CHANGAMOTO
Tamaduni za ndaki ya COET
zisizoruhusu mtu yeyote asiyemhandisi kupanda katika kimbweta ili kuhutubia,
huenda zikaamsha hasira kwa watu wa ndaki zingine kwa kujihisi wamedharauliwa
na hivyo kumnyima kura.
Pia, Inasemekana ni kada mwaminifu
wa CCM, lakini anaonekana kuwahadaa wanaDARUSO kuwa yeye ni mpinzani. Uongo
kama huu, ukishindwa kumfaidisha, utamwangusha.
Pia, Anaungwa mkono na viongozi
wengi wa serikali dhaifu iliyopita. Huenda watu wakadhani hana jipya kwani naye
alikuwa mmoja wa serikali hiyo.
*Nguvu kubwa inayotumiwa na
wafuasi wake, mabango mengi yaliyotapakaa kila mahali, na utekaji mkubwa wa
mitandao ya kijamii, unafaida kubwa kwake. Hivyo basi, apige pasi suti yake,
huenda akawa rais
#Makoba