VICHEKESHO VILIVYOTUFIKIA WIKI HII
Leo tupo kwenye Taxi tunaelekea
Mjini Traffic akasimamisha gari letu, akamuuliza Dereva "Mbona plate namba
za nyuma na mbele ni tofauti !?. Dereva akamjibu, 'Kwani ww sura yako na
makalio yako vinafanana !?.
Wote tukaanza kucheka ...
Tumepandishwa kwy defender lao
nadhani wanatupeleka kupata lunch !
πππππππππ
XXX
π€π€π€π€
IVI KWA MFANO MKEO
AKIWA NA KICHWA KIKUBWA KULIKO WW
BADO TU UTAITWA KICHWA CHA FAMILIA?
π€£π€£π€£π€£π€£
XXX
......... Jaman Hivi hakuna Mtu yeyote
Mwenye *Picha* ya *WAHENGA* Anitumie
Mimi Nawaskiaga Tu Cjawahi kuwaona
πππππ
XXX
Ile siku nitaona mwanamke akiskuma
mkokoteni bila shati.....ndio nitaamini
kuwa
#what_a_man_can_do_a_woman_can_do_better πππ
Wacha niende hivi narudi baadae
ππΌππΌππΌππΌ
XXX
Mdada:- beby nimefukuzwa kwetu
Jamaa:- maskini pole
Mdada:- Hapa Hata sijui ntafanyeje
Jamaa:- panda Gari za mbagala zinazopitia
Tazara ulale kwenye FoleniππΎππΎ
XXX
Mwalimu: *Alex, simba akianza kukufukuza
utafanya nini?*
Alex: *nitapanda juu ya mti.*
Mwalimu: *je na simba nae akipanda juu ya
mti?*
Alex: *nitakimbilia mtoni niogelee.*
Mwalimu: *je simba nae akikufuata mtoni?*
Alex: *mwalimu uko upande wangu au wa simba?
Maana* *sikuelewi kabisa, kila ninavyojaribu kumkwepa* *simba we unamwelekeza
niliko, kama hunipendi sema tu.*
π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£π€£
XXX
*Binti anakula chapati tano na maharage robo
harafu ww bado unamuita baby huyo ni brother*
C & P
XXX
Kama hujawahi kupata 100% ulipokua Shule ya
msingi, na Secondary, basi tambua kuwa 100% pekee ambayo utaweza kuiona
maishani mwako ni pale simu yako ikiwa imejaa chaji 100%.πππππππ
XXX
*BABA*: mwanangu mbona skuizi wapenda niita
DAD badala ya BABA
*BINTI* : kuita baba kunamaliza lipstick.
ππππππππ
XXX
*nahitaji msaada wenu jamanii..*
nipo hapa ubungo nataka kwenda China
kumsalimia Jack Chan.., nipande gari za wapi..!!!??
XXX
Nawapenda Sanaa wanawake wa uswahilini kwa
ubunifu wao. Hivi ni baadhi ya vicheko walivyo Cheka kwenye miaka tofauti.
2002 to 2004- walikua wanacheka "hehehe
haloooo"
2005 to 2007- wakaja Na "hehehe
utajiju"
2008 to 2010- wakaleta hii ya "hehehe
unalooo"
2010 to 2012- wakaleta "hehehe
utajibeba"
2012 to 2014- wakaja Na "hehehe
kaoge"
2014 to 2015- SAFARI hii hapa wakacheka
"hehehe chezea mie wewe"
2016- hapa sasa ndo wamekuja Na ..... Hehehe
kantangazeeeeee
2017- wamekuja Na hii hapa "hehehe
warere wapi nyonyoo.
Jee una hisi 2018 watabuni style gani ya
kucheka ππππππππππππ
XXX
*kumbukumbu ya kusikitisha*ππ
*Tarehe kama ya leo miaka mitano iliyopita
muuza karanga alikimbia na chenchi yangu*
ππ
XXX
NIKIWA SHULE MWALIMU WANGU WA KISWAHILI
ALINAMBIA "MTU MWENYE MKONO MREFU MAANA YAKE NI MWIZI"
SASA KUNA WAKATI UNASIKIA VIONGOZI
WANASEMA..MSICHEZE NA SERIKALI MAANA SERIKALI "INA MKONO MREFU"
*YAANI HAPO NDO NASHINDWAGA KUELEWA NDUGU
WATANZANIA*πππππ
XXX
Kama hujawahi kuongea Kichina basi hii ni
nafasi pekee ya
kufanya mazoezi.....,......rudia kwa haraka
haraka ...
"MY SHOE SHALL SOON SHINE"
Tuma audio please angalau tucheke
kidogo.....
ππππππππππππππππ
XXX
*Jamaa yupo kwenye daladala pembeni kuna
mrembo mkali kakaaa.Akamlia timing afu akamuuliza*
jamaa:Samahani dada hivi unaitwa "Google"
Demu:hapana..kwa nini?!
jamaa;Una kila kitu ninachokitafuta.
π
π
πππ
ππππ
XXX
*Maisha yamekaza hadi unamuuliza mkeo kama
ana boyfriend awakopeshe hela? Na stress
ni pale anapokujibu kwani ulikuwa unataka kiasi gani nimuulize?
...napita tu...πππ
XXX
*Wanyama wangekuwa na WHAT'S UP.*
Status zingekuwa:
MENDE: "nimekoswa na guu la mama mwenye
Nyumba, maisha yangu mashakani, why always me???? "
PANYA: "nimekula nguo lenye pafyumu,
nasikiaje kiu. uwiiiii"
NGURUWE: Binadamu wabaya jamani,
wameshanizushia nasambaza mafua "
MBU: Nina HIV, nimekomaje kunyonyanyonya
hovyo.
MBUZI: teh teh teh. thank Good pasaka
imepita. ni kula BATA tuu mpaka EID.
KUKU: "friends mkiona kesho kimya mjue
nipo mezani maana kuna wageni wamekuja leo hapa home, tuombeane uzima wapendwa,
love you all"ππππππ
XXX
*πEnzi hizo shule kuna wanafunzi walikuwa wanaandika topic kwa kalamu
nyekundu, sub topic kalamu ya nyeusi, na
notes kalamu ya bluu.π Sijui mko wapi siku hizi, au mlipata kazi
sadolin?*
πππππ
XXX
*boy* : *baby* *nataka* *niwe* *pirot*
*girl* : *acha* *tu*
*boy*: *kwanini* *unasema* *hivyo*
*girl* : *yani* *umeshindwa* *kulusha*
*vocha* *utaweza* *ndege* π€π€π€π€π€π€π€
*girls* *shikamooo*
XXX
Bwana alikua ameketi na wake zake wawili
sitting room waangalia TV pamoja. Akawa anasikiu kiu lakini akaona ni hishima
kumtuma yule bibi mdogo. Alipokua amekwenda kuleta hiyo glassi ya maji, bibi
was kwanza akaanza;
"Sasa ndio wanionesha nini! kama ni
maji basi sote twajua kuteka. Ama wataka kumwangalia mwendo tu akenda na
akirudi kuni dhalilisha mimi. Sawa lakini mungu yuko, dhalimu mkubwa wewe huna
uadilifu mwanamume wewe basi tu"π³
Bibi mdogo akirudi na glassi yake ya maji
nae akaanza;
"Haya musha zungumza hiyo siri yenu!
najua uliku waniondoa ki hikima mupate kunisengenya lakini inshallah mungu
atawashinda na dhulma zenu hizo"π³
Heri angebaki na hio kiu yake maskini
ππ€£ππ€£ππ€£
XXX
XXX
```Je, wajua...```?
*Katika maisha yake yote ya _Adolf Hitler_*
*hakuwai kusema neno Ahsante na yote hii ni kutokana na kutojua kuongea kiswahili*
π
π
π
π
π
π
π
π
_Sio lazima tuelewane bhana_
Vichekesho hivi vyote vimechukuliwa kutoka mtandao wa WhatsApp. kwa bahati mbaya watunzi wake wengi hawafahamiki kwa sura wala majina.