HII HAPA ‘TWEET’ YA OBAMA ILIYOONGOZA KWA ‘LIKES’
Hii ni Tweet ambayo imeongoza kwa kupata
‘likes’ nyingi zaidi katika mtandao wa ‘twitter’.
Katika ‘tweet’ hiyo, Obama amenukuu maneno matatu yaliyowahi kusemwa na rais wa zamani na mpigania uhuru wa Afrika ya
Kusini – Nelson Mandela. Pia ‘tweet’ hiyo, ina picha ya Obama akiwa na watoto wenye asili tofauti, wakitabasamu kwa pamoja.
Kwa sababu ya uvamizi uliotokea
Charlottesville, Virginia, imepata zaidi ya ‘likes’ milioni tatu.
Picha inayoambatana na ‘tweet’ hiyo
ilipigwa mwaka 2011 na aliyekuwa mpiga picha wa ikulu, Pete Souza.
‘Tweet’ hiyo inasema, ‘hakuna mtu
aliyezaliwa akimchukia mtu kwa sababu ya rangi yake ya ngozi, historia au dini
yake.