KOLABO YA CHID BENZ NA TUPAC ILIVYOJADILIWA MITANDAONI
![]() |
Chid Benz ameamsha hisia za
watu mbalimbali, maarufu na wasiomaarufu baada ya kudai amemshirikisha marehemu
Tupac Shakur katika wimbo wake mpya na hivi karibuni atamleta nchini hapa ili
watu wamuone.
Alizidi kueleza kuwa, Tupac
hajafa bali yuko Cuba na huko ndiko alikofanikiwa kufanya naye Kolabo hiyo ya
wimbo anaotarajia kuuachia.
KIKI AU MADAWA
Baada ya video hiyo
kuonekana, watu mbalimbali wametoa maoni yao kuwa inawezekana amefanya hivyo
akiwa na akili zake timamu kwa lengo la kupata ‘kiki.’ Wengine wametupia lawama
madawa ya kulevya kwani Chid ameshindwa kabisa kuachana na matumizi ya madawa.
WALICHOANDIKA MASTAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
“Msipowapandisha hawa watu
(Chid Benz na Tupac) Fiesta hatutaelewana.” Edo Kumwembe.
Naye msanii Madee aliandika
msimamo wake kuwa, ndiyo sababu kubwa huwa hataki hata kuvuta sigara.
Itakumbukwa kuwa, siku
chache zilizopita Chid alikamatwa kwa sakata la madawa ya kulevya na kuwekwa
chini ya uangalizi mkali wa mahakama.
Unalizungumziaje hili? shusha Comment yako...