MAJARIBIO YA KOMBORA LA KOREA YASABABISHA MADHARA
Picha za Satelite
zilizopigwa, zimetoa majibu juu ya madhara yaliyosababishwa na majaribio hayo.
Korea kasazini ambayo ni kinara wa majaribio ya makombora ya Nyuklia,
imesababisha mmomonyoko mkubwa wa ardhi ukiambatana na utelezi.
Korea ya Kaskazini imefanya
majaribio sita ya nyuklia. Taarifa zimethibitisha kuwa, picha za hivi karibuni
zinaonyesha mmomonyoko mkubwa wa udongo na utelezi katika maeneo yalikotumwa
makombora.
Uharibifu huo umetokea
katika eneo la mlima Mantap. Pia wataalamu wameeleza hali hiyo inaweza
kusababisha mlipuko wa volcano.
Korea Kaskazini imekuwa
ikiendesha majaribio mengi ya Nyuklia suala ambalo haliungwi mkono na mataifa
mengi ikiwemo Marekani.
IMEANDIKWA NA: MOWASHA|
NGEME