Sababu za Fasihi Kuwa Sanaa na Tofauti Yake na Tanzu Nyingine za Sanaa
Kwa vipi fasihi ni sanaa?
Sanaa ni uzuri unaojitokeza
katika umbo lililosanifiwa ambapo mtu hulitumia umbo hilo kueleza yale
anayotaka wengine wayafahamu.
i.
Matumizi
ya mtindo katika kufikisha ujumbe. Mtindo humtofautisha mwanafasihi mmoja na
mwingine. Kila mwanafasihi ana mtindo wake. Ufundi unakuja pale ambapo ufundi
hutumika katika mtindo ambapo mambo kama, matumizi ya barua, dayolojia,
monolojia na matumizi ya nafsi hujumuishwa.
ii.
Matumizi
ya muundo. Jinsi ambavyo visa hupangiliwa kwa ufundi mkubwa ili kuwezesha
kuifikisha kazi ya fasihi kwa walengwa, ndiyo sanaa yenyewe. Maana yake ni
kwamba, mwandishi hutumia ubunifu katika kupangilia visa na matukio.
iii.
Matumizi
ya lugha. Lugha itumikayo katika fasihi ni tofauti na lugha nyingine. Katika
lugha ya fasihi kuna matumizi ya tamathali za semi, misemo, nahau na ujenzi wa
picha na taswira. Haya yote yanaifanya fasihi iwe sanaa.
iv.
Matumizi
ya wahusika. Si kutumia wahusika pekee, bali ule uchaguzi mzuri wa wahusika
huifanya fasihi iwe sanaa. Mwanafasihi anauwezo wa kuamua anataka wahusika wa
aina gani katika kazi yake. Ana uwezo wa kumwacha hai mhusika mpaka mwisho wa
kazi yake. Pia, ana uwezo wa kuyakatisha maisha ya mhusika yeyote.
v.
Matumizi
ya mandhari. Jinsi mwandishi anavyojenga mandhari yake kwa ubunifu ndiyo
huifanya fasihi ikawa sanaa. Kadiri mandhari inavyojengwa na mwandishi ndivyo
inavyosaidia kuijenga kazi ya fasihi na kuifanya ieleweke zaidi kwa wasomaji.
Tofauti ya fasihi na tanzu nyingine za sanaa
Fasihi na tanzu nyingine za sanaa
kama uchongaji, ususi, utarizi, muziki, ufumaji, uchoraji, ufinyanzi na
maonyesho vinatofautiana kwa kiasi kikubwa kama ilivyoorodheshwa katika hoja
hizi:
-
Kazi
za fasihi hutumia lugha.
-
Kazi
za fasihi hutumia wahusika.
-
Kazi
za fasihi hutumia mandhari.
-
Kazi
za fasihi huwa na utendaji. Huu hujitokeza zaidi katika fasihi simulizi,
ambapo, fanani na hadhira yake hutenda.
-
Kazi
za fasihi zina fani na maudhui.