SERIKALI YAOMBWA KUAJIRI WAALIMU
Huko Mwanza Serikali
imetakiwa kuajiri waalimu wa kutosha ambao watasaidia vyuo mbalimbali kufikia
viwango vya ufundishaji. Haya yamejiri baada ya kuwepo kwa madai ya muda mrefu
katika vyuo vya mafunzo ya wauguzi na wakunga (Manesi).
Vyuo mbalimbali vya utoaji
wa mafunzo haya nchini vina upungufu mkubwa wa waalimu jambo linalorudisha
nyuma ufanisi na ubora wa elimu inayotolewa.
Mkurugenzi mtendaji wa chuo
cha mafunzo ya uuguzi, Ndemetria Vermand alisema: “Ni kweli vyuo vyote binafsi
na visivyo binafsi vina uhaba wa walimu, lakini tatizo hili ni kubwa zaidi kwa
vyuo vya serikali.”
Alizidi kusisitiza hayo
kuwa, utoaji wa huduma hizi utasaidia katika ubora elimu ya afya inayotolewa
nchini.
Mdau mwingine wa huduma za
afya, Molland Makamba alisema kuwa kuna vyuo 161 vya mafunzo ya Uuguzi na kati
ya hivyo, 77 vinamilikiwa na serikali.
Hayo yote yalijiri katika
hafla ya utoaji wa vyeti na tuzo kwa wafadhili watatu wa USAID ambao wamekuwa
wakisaidia vyuo vya mkoani Mara na Kagera.
NA: MOWASHA| NGEME