Sheikh Ponda Atii Agizo la Kamanda Mkuu wa Polisi Mambosasa
Siku chache zilizopita kamanda
mkuu wa jeshi la polisi bwana Mambosasa alimwagiza Ponda ajisalimishe katika
kituo chochote cha polisi kutokana na kauli yake iliyodaiwa kuwa ya kichochezi.
Katika kukubaliana na kauli hiyo,
Ponda amewasili kituoni akiambatana na wakili wake, Abdallah Safari.
Hayo yote yamejiri baada ya
mkutano aliofanya na vyombo vya habari siku ya Jumatano. Baadhi ya matamshi
aliyotoa, ndiyo yanayosemwa kuwa ya kichochezi.
Hii si mara ya kwanza kwa Ponda
kupewa tuhuma hizi. Mara kadhaa ametuhumiwa kwa uchochezi na hata kutupwa
rumande kwa muda mrefu. Hata hivyo, katika mara zote hizo alipatikana akiwa
hana hatia.