Uhusiano wa Fasihi na Tanzu Nyingine za Sanaa

Uhusiano wa Fasihi na Tanzu Nyingine za Sanaa| Sekondari na Vyuo
Fasihi ni taaluma inayotumia sanaa maalum ya lugha. Nayo SANAA ni uzuri unaojitokeza katika umbolililosanifiwa, umbo ambalo mtu hulitumia kueleza hisi zinazomgusa kwa kutoakielelezo au vielelezo vyenye dhana maalum. Ukiachilia mbali fasihi, baadhi ya tanzu nyingine za sanaa ni: Ususi, utarizi, sanaa za maonyesho, ufinyanzi, uchoraji na uchongaji. Upo uhusiano wa fasihi na tanzu hizi za sanaa kama inavyoelezwa:
Zote ni kazi za sanaa. Kama ufinyanzi, uchoraji na uchongaji ulivyo, yaani uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa, umbo ambalo mtu hulitumia kueleza hisi zinazomgusa kwa kutoa kielelezo au vielelezo vyenye dhana maalum.
Fasihi na tanzu nyingine za sanaa hutoa mafunzo fulani. kwa mfano, katika kazi ya fasihi andishi ya WATOTO WA MAMAN’TILIE, tunapata mafunzo kuwa, ulevi si suluhisho la matatizo. Pia, katika sanaa nyingine kama sanaa za maonyesho, kuna mafunzo ambayo watazamaji huyapata.
Fasihi na tanzu nyingine za sanaa hutegemea watu. Riwaya, tamthiliya na ushairi hutegemea watunzi na wasomaji. Fasihi simulizi hutegemea fanani na hadhira. Ususi hutegemea mtu mjuvi wa huo ususi, katika ununuzi hutegemea wateja. Uchongaji nao vivyo hivyo, pasi na mchonga vinyago na mnunuzi wa sanaa hiyo, hakuna kitakachoendelea.
Yapo mengi sana yanayofanya fasihi na tanzu nyingine za sanaa zihusiane. Hata hivyo, hii haina maana kuwa fasihi na tanzu nyingine za sanaa hazina tofauti.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2025

Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 1