Mtihani wa Kiswahili 1 Kidato cha Sita| Pre necta| Dec 2017
Muda: saa 3
Maelekezo
1. Mtihani huu una maswali saba katika sehemu A, B, C, D na
E.
2. Jibu maswali yote.
JINSI YA KUUFANYA MTIHANI HUU
Mtu yeyote na kokote aliko
anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume
WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba - 0754 89 53 21.
Subiri mtihani wako usahihishwe. Urudishiwe na
ufanyiwe masahihisho.
Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000 tu.
Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 na Tigo
pesa 0653 25 05 66
“Kwa kuwa lengo la mtihani huu ni kutaka kujua uwezo
na mapungufu ya mwanafunzi ili aweze kupewa mbinu mbadala za kumsaidia kufaulu
mtihani wake wa mwisho, kuangalizia majibu hakuna faida yoyote kwani lengo la
mtihani si kubaini nani atakuwa wa kwanza na yupi atakuwa wa mwisho!”
Daud Makoba – Mwalimu Makoba – Mwalimu wa Waalimu.
Unataka kufanya mtihani huu na hujaelewa taratibu
zake? Wasiliana na Mwalimu Makoba kwa 0754 89 53 21.
Sasa fanya mtihani wako.
SEHEMU A (Alama 20)
UFAHAMU
1. Soma kwa makini kifungu hiki cha habari kisha jibu
maswali yanayofuata.
UTUPU ni hali ya kutokuwa na
kitu. Huenda ukawa utupu wa pochi, chumba, mali, akili na hata utupu wa mwili.
Wahenga wa zamani (sio hawa wa mitandaoni), waliupuuza utupu kwa kusema, Mkono
mtupu haurambwi.
Hali ya utupu hivi sasa inazidi
kubadilika kwa kasi. Utupu umegeuka kitu. Utupu unategemewa kumvusha mtu kutoka
sehemu moja kwenda nyingine.
Tazama nyimbo za wanamuziki zilivyo.
Wasichana wanaotumika humo wanacheza
utupu kabisa. Hawaogopi lolote na hata aibu hawaoni.
Zamani wazee walipotaka kumwaga
laana, walitishia kuwaonesha watoto wakorofi utupu. Enzi hizo kuonekana kwa
utupu ilikuwa ni laana kubwa. Wapo ambao walichanganyikiwa na kuwa wehu kwa
sababu ya kadhia hii.
Vibinti vya zama hizi vinapiga
picha za utupu bila kuogopa chochote. Ukiviuliza kwa nini vinafanya hivyo,
utasikia vinajibu kuwa vinapenda kuwa hivyo… vinapenda kukaa utupu. Ujinga
mtupu.
Hali ya mabinti kukaa utupu kwa
kiasi kikubwa imepunguza hamu ya vijana kuoa. Ndio, vijana wanaona kila kitu.
Sasa aoe ili aone nini kingine.
Maadili yamebadilika sana sasa.
Ni kweli kuwa hapo zamani mwanadamu alitembea utupu. Lakini tamaduni hubadilika
kulingana na wakati. Mwanadamu tangu kupata ustaarabu wake, utupu si jambo la
kuonyesha hadharani.
Bado ninaendelea kutafakari nguvu
hii ya utupu kukamata hisia za watu imetoka wapi? Ni kweli wanaowachezesha
mabinti wakiwa watupu namna ile watafurahi wakiwaona watoto wa kuwazaa wao
wakifanya vile? Lazima sasa turejee katika maadili. Heshima iwepo.
Jamaa mmoja aliwahi kunieleza
kuwa, utupu kuzidi kuonekana mara kwa mara kumemwaga laaana kali katika jamii.
Ndiyo maana kila kukicha limeibuka lile, mara limetokea hili.
Sina uhakika kama kuna sheria
inayoeleza lolote kuhusu mavazi. Ni wakati wa kulitafakari hili kabla hali
haijawa mbaya zaidi.
Ni utupu wa fikra kuamini kuwa
utupu unaweza kukupatia mafanikio. Sana utaambulia, kupata umaarufu wa mpito.
Maswali
a. Toa maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika
habari uliyoisoma.
i.
Wahenga.
ii.
Laana.
iii.
Sheria.
iv.
Zama.
v.
Tamaduni.
b. Mwandishi ana maana gani anaposema “waliupuuza utupu
kwa kusema, Mkono mtupu haurambwi.”
c. Unaelewa nini kuhusu mabinti wa zama hizi? Toa maelezo
kwa mistari isiyozidi mitatu.
d. Kwa kutumia aya ya tatu, mwandishi ana mtazamo gani
kuhusu wanamuziki.
2. Fupisha habari uliyoisoma kwa maneno 100.
SEHEMU B (alama 20)
SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA
3. Katika tungo zifuatazo taja kielezi na fafanua aina ya
kielezi hicho.
i.
Hospitali
imefungwa kwa mara ya saba.
ii.
Amekaa
juu ya ndoo.
iii.
Anapigana
kishujaa.
iv.
Nitaondoka
asubuhi na mapema.
v.
Mwanenu
ameelekea upande wa kushoto.
4. Ni kwa vipi lugha ya Kiswahili inafaidishwa na
rejesta? Toa hoja tano.
SEHEMU C (alama 20)UTUNGAJI
5. Jifanye wewe ni meneja wa kiwanda cha kufyatua
matofali S.L.P 700 Kigoma, andika barua ya kumpa ruhusa ya siku tatu mfanyakazi
wako aitwaye Kitalula Abubakari S.L.P 1223 Kigoma. Jina lako liwe Chimatu
Baraka.
SEHEMU D (alama 20)MAENDELEO YA KISWAHILI
6. Lahaja ya Kiunguja ilikidhi vigezo fulani hata
ikasanifishwa kuwa Kiswahili tukionacho leo. Ni masharti yapi yalifikiwa na
lahaja hii hata ikaweza kupitishwa? Toa hoja tano.
SEHEMU E (alama 20)TAFSIRI NA UKALIMANI
7. Tafsiri na ukalimani ni dhana ambazo zimekuwa
zikichanganywa mno na watu. Tumia maarifa uliyoyapata katika kozi hii, kuondoa
utata huo. Toa hoja nne.