Sitasahau Nilipolala na Mwanamke Juu ya Kaburi (28)| Riwaya
Nikiwa nimekaa katika kiti
kimojawapo miongoni mwa viti vile vinne, mlango ulifunguliwa. Aliyefungua
mlango ule ndiye aliyeingia. Alikuwa msichana nisiyeweza kutambua umri wake.
Hata hivyo, aliumbwa vyema akaumbika. Kiunoni alivaa ngozi fupi hivyo
nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuuona uzuri wa mapaja yake ya rangi ya kunde.
Nilipoyaona manyoya laini ya kike chini kidogo ya kitovu chake, damu ilikwenda
kasi na kunifanya nisahau kabisa kama nilikuwa mateka.
Alikuwa na sura ndogo tamu, nyusi
nyingi na midomo minene, kifuani paliinama na hapakuwa na mpango wa kudondoka.
Fahari ya macho ni kwamba, kifuani hakufunga chochote! Mkono wa kushoto alibeba
birika dogo, kulia alikamata sahani kubwa iliyokuwa na mapaja manne makubwa ya
kuku waliokaangwa na mpishi stadi. Alitembea taratibu kwa madaha kama mlimbwede
anayelitaka taji. Akili yangu haikufanya kazi nyingine isipokuwa kushangaa kwa
uchu. Macho niliyatoa pima!
Alifika na kuweka birika na nyama
juu ya meza. Nilishindwa kujizuia, nikamchombeza.
“Bibie waitwa nani? Mbona
vururuvururu bila hata ya salaam!”
Maneno yangu hayakujibiwa.
Aliachia tabasamu pana ambalo lilizidi kunimaliza kisha akatembea kuelekea
mlango aliotumia kuingia. Sehemu za nyuma zilitikisika isivyokawaida,
niligundua alifanya makusudi ili anichanganye. Masikini mateka mimi,
nilitetemeka kwa uchu!
Niliishambulia nyama ya kuku na
maziwa. Hakukuwa na kikombe, nilikunywa maziwa yakiwa ndani ya birika. Raha
iliyoje.
Matunzo niliyopewa
yalinichanganya na kunifanya nitafakari ni kwa nini nilifanyiwa vile. Kwa ujuvi
nilionao, mateka wa aina yangu huteswa vilivyo kiasi cha kujuta na kutamani
kufa. Kwangu ilikuwa tofauti.
Maisha yaliendelea nikiendelea
kutunzwa vyema. Nilipewa vyakula vya kila aina hata nikastaajabu mambo haya.
Hakika nchi hii ilikuwa ya uki na maziwa, nilinawiri matekani.
Ilikuwa asubuhi ya siku ya saba
tangu niwe mateka katika nchi ya Matumbawe. Msichana anileteaye chakula
aliingia. Siku zote aingiapo humsemesha asinijibu. Niliandaa kisa cha kumpima.
Alipoingia nilikuwa katika kiti nimekaa. Macho yetu yalipogongana,
nikatengeneza hasira bandia kisha nikanyanyuka na kujitupa kitandani. Aliweka
birika la maziwa na nyama ya kuku mezani na kunifuata nilipolala.
“Una shida gani leo?” aliuliza.
Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kuisikia sauti yake. Ilikuwa sauti laini
nyembamba ya kike haswaa. Bila shaka sauti hii ingeweza kumtoa nyangumi
baharini!
Sikumjibu, nilinyanyuka kwa
hasira nikaenda kukaa katika kiti. Alinifuata na kuniuliza swali lilelile la
awali. Sikumjibu. Nilinyanyuka tena nikiwa nimekunja sura na kwenda bafuni.
Hakunifuata! Nilibaki bafuni kama zuzu ananyolewa ndevu!
Niliamua kurudi. Nilimkuta kakaa
juu ya kiti kajiinamia kwa hudhuni. Nilimsogelea na kumuuliza tatizo.
Hakunijibu, alirusha mikono na kuanza kuondoka. Nilisimama nikamkamata, haraka
bila kuchelewa nikaibusu midomo yake. Alitaka kunizuia, lakini mwili haukuweza
tena, alipumua kwa hisia kali na kunifanya nijipongeze kwa ushindi. Nikaongeza
busu tena na tena, nikaona sasa mambo yamewiva. Nilimsogelea zaidi, hakuwa na
pingamizi. Midomo yangu na yake ikakutana, bila kujitambua tukaanza kunyonyana
ndimi zetu. Alihema juujuu. Nikaongeza ujuzi. Niliuruhusu mkono wangu umpapase
kila mahali, nilipofanya hivyo, miguno ya kimahaba ilimtoka. Sikuwa na muda wa
kupoteza. nilimbeba mzimamzima na kumbwaga kitandani. huko ningenyonya zile
chuchu imara na kuchota maji kisimani.
Itaendelea Jumanne…
“Si ruhusa kuchukua hadithi hii na kuiweka katika mfumo wa sauti, kutoa kitabu, kuweka katika blogu au ‘website’ nyingine, au kufanya chochote kile bila kuwasiliana na mmiliki! Hatua kali zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayekiuka!”
Daud Makoba 0754 89 53 21