Tanzania Kifua Mbele, Yatofautiana na Kauli ya Donald Trump
Siku
chache zilizopita, Donald Trump ambaye ni rais wa Marekani alitoa kauli tata
ambayo ilikutana na ukosoaji mwingi zaidi kuwahi kutokea. Trump alidai
anautambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa taifa la Israel.
Baada
ya nchi nyingi ikiwemo Saudi Arabia kupinga kauli hiyo, Tanzania nayo
imejitokeza hadharani na kutofautiana nayo.
Wizara
ya mambo ya nje ya Tanzania imesema inaunga mkono makubaliano ya kimataifa
ambayo yanatambua haki ya watu wa Palestina ya kumiliki mashariki wa Jerusalem
kama ilivyokuwa kwenye mpaka wa kabla ya mwaka 1967.
Taarifa
iliyotiwa saini na Waziri Mahiga ilisema, “Tanzania
inaunga mkono msimamo wa Umoja wa Mataifa wa suluhu ya mataifa mawili ambayo
unatoa nafasi ya Israel na Palestina kuwepo kwa pamoja zikiwa na mipaka salama."
Msimamo wa Tanzania unakwenda pamoja na
msimamo wa mataifa mengi ulimwenguni.
Kauli ya Trump imetajwa na wachambuzi wengi
kuwa ni yenye utata na inayoweza kusababisha kukosekana kwa amani zaidi katika
eneo la Israel na Palestina.