Mtihani wa Kiswahili Kidato cha Tatu Annual | Past Papers
Photo Credit: ZanziNews |
1.
Soma kifungu hiki cha habari kisha jibu
maswali yanayofuata:
ANA
wajukuu wanne, umri wake ni miaka 70, na kila mmoja hushangazwa na muonekano
wake! Ni bibi asiye mzee. Ajabu kubwa.
Siri
pekee inayomfanya awe na muonekano huo ni aina ya vyakula anavyokula na
kuzingatia mazoezi ya kutosha. Anazingatia anachoweka mdomoni na miguu yake
haiishi kutembea.
Bibi
huyu, anayetokea Perth, Australia, wakati alipokuwa na umri wa miaka 40
alitahadharishwa na madaktari kuwa endapo angeshindwa kubadili mtindo wa
maisha, punde angeugua maradhi ya kisukari. Ili
kuokoa maisha yake, akaamua kuvipa
kisogo vinono vyote, na huo ndiyo ukawa mwanzo wa maisha mapya. Ni mwanzo
huu unafanya tumzungumzie! Siri ya Bi Carolyn Hartz kuonekana kama binti mdogo.
Ukiachilia
mbali vyakula sahihi anavyokula, hulala kwa muda wa saa saba, kujishughulisha
na kazi zake binafsi siku nzima, na kama ilivyo asili ya wanawake wengine,
hutumia muda kiasi kujipamba. Kipo cha kujifunza kutoka kwa bibi huyu.
i.
Kipi kinafaa kuwa kichwa cha habari hii?
ii.
Taja siri pekee inayomfanya Bi Caroly Hartz
kuwa na mwonekano alionao sasa?
iii.
Toa maana ya neno kuvipa kisogo vinono vyote.
iv.
Kwa mujibu wa kifungu hiki cha habari,
unafikiri ni ipi njia sahihi ya kufukuza maradhi?
v.
“Kipo cha kujifunza kutoka kwa bibi huyu.”
Taja mafunzo manne uliyoyapata.
2.
Fupisha habari hiyo kwa maneno yasiyozidi 60
SEHEMU B (alama 30)
3.
Toa maana ya upatanishi wa kisarufi. Weka
mifano minne.
4.
Ni ipi tofauti ya kirai na kishazi? Kwa
kuzingatia mifano, toa tofauti mbili kwa kila moja.
5.
Kwa kutumia kigezo cha kimuundo, taja aina
tatu za sentensi. Toa mifano kwa kila aina.
SEHEMU C (alama 20)
6.
Wewe ni mfanyabiashara wa vipuri vya magari.
Andika tangazo la biashara yako litakalochapwa katika gazeti la MWENDAKWAO
litokalo kila Jumamosi.
7.
Andika barua ya maombi ya kazi ya ulinzi
katika mgodi wa Buzwagi. Tumia ubunifu wako kuweka jina na anuani ya
unayemwandikia.
SEHEMU D (alama 10)
8.
Thibitisha mfanano wa kimsamiati wa Kiswahili
na lugha nyingine za kibantu
SEHEMU E (Alama 30)
9.
Tunga ngonjera kuhusu kisa kisemacho, MJINI
NI BORA KULIKO KIJIJINI.
10.
Tumia riwaya ya Watoto wa Maman’tilie
kuthibitisha jinsi watu wazima wanavyoshindwa kutimiza wajibu wao katika jamii.