Maswali Katika Riwaya ya Takadini
Jibu maswali yote
1. Chagua jibu sahihi
i. Takadini anataka kuuliwa na jamii yake kwa sababu ya
a. Dhambi za Sekai b. Mila na desturi c. Amri ya mizimu d. Kutoitakia mema nchi yake
ii. Ni kipi chanzo cha mgogoro wa Shingai na wazazi wake
a. Kukataa kuolewa na Takadini b. Kukataa kuolewa na Nhamo c. Uvivu na uzembe wa kazi d. Lugha chafu
iii. Alimpiga mkewe kila siku kwa sababu alimwona dhaifu na duni
a. Nhariswa b. Dadrai c. Manyamombe d. Mukaru
iv. Mwandishi wa riwaya ya Takadini ni
a. Mussa Banzi b. Penina Mhando c. Vivian Mmari d. Ben Hanson
v. Riwaya ya Takadini ilipata kuandikwa huko nchini
a. Zimbabwe b. Tanzania c. Malawi d. Cameroon
2. Andika kweli au si kweli
i. Walemavu wana haki ya kuishi kama watu wengine
ii. Ujasiri utaondoa unyanyasaji wa watu wenye ulemavu
iii. Dadrai ana.anamzalia Takadini mtoto asiye ba ulemavu wowote.
iv. Riwaya ya Takadini imetumia wahusika wa kiume pekee.
v. Nhamo ana mapenzi ya kweli kwa Takadini.
3. Ni ipi falsafa ya mwandishi Ben J Hanson
4. Jadili sababu nne za mgogoro wa Nhamo na Takadini
5. Yaliyotokea katika kitabu cha Takadini yana uhusiano wowote na jamii yako? Jadili.