Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi. CV au wasifu ni kitu cha lazima kwa yeyote anayeomba kazi. Watu wengi wanaokosa kazi, tatizo huwa siyo wao, bali tatizo huwa ni CV zao. Kumekuwa na makosa mengi katika uandishi wa CV jambo ambalo limesababisha watafuta kazi wengi kushindwa kuitwa kwenye usaili. Makala hii itakueleza namna sahihi ya kuandika CV, utaitwa katika ‘interview’ nyingi endapo utaandika CV sahihi. Tena nakukumbusha, kila taaluma ina aina yake ya CV, CV ya rubani haifanani na CV ya injinia. Vivyo hivyo, CV ya mpishi haifananani na CV ya Mwalimu. Pia nakukumbusha usome jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi , kwani CV huenda pamoja na barua ya maombi ya kazi. CV Bora ni Ipi? Ukurasa Mmoja au Kurasa mbili hadi tatu? CV bora ni ile yenye kurasa mbili hadi tatu. Watu wengi wanapojifunza namna ya kuandika CV, wamekuwa wakiona CV zenye ukurasa...
Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi. Umewekeza katika elimu yako, una kila sifa ya kupata kazi fulani lakini hupati kazi hiyo, inawezekana kabisa sababu mojawapo inayokufanya usipate kazi unayoitaka ni kutokujua kuandika barua ya maombi ya kazi au unapoandika, unaandika katika namna mbaya inayofanya waajiri wakupuuze. Kwa muda mrefu nimekuwa nikiulizwa na wanafunzi na wasomaji wa mtandao wangu kuhusu jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi kwa kiswahili, na wengine huuliza kuhusu jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi kwa kiingereza. Waombaji wengi huuliza kuhusu maombi ya kazi ya udereva, hotelini, kazi za polisi, ualimu, afya utendaji wa kijiji na kazi chungu nzima ambazo haziwezi kutosha hapa zikiandikwa. Kazi zote siku hizi zinahitaji kuandika barua, hata kama unataka kujitolea, lazima utaandika barua! Isivyo bahati ni kuwa, hata mtandaoni ...
1. Kukosa hela ni vibaya sana, unaweza kukutana na ng’ombe ukahisi wanakusema. 2. Kama huna gari , huna nyumba, huna simu na huna hela, tofauti yako na kenge ni mkia. 3. Siyo kila anayeamka saa sita mchana ni tajiri, wengine wanapunguza saa za kuteseka. 4. Mtu mmoja aliota anaendesha gari, ikakwama kwenye matope, akaanza kuisukuma. Alipoamka, akajikuta yupo na kitanda jikoni. 5. Maisha ni ya ajabu sana, unakuta mtu hajaoa lakini chumba anachoishi kuna panya wana familia zao na yeye ndiyo anawalisha. 6. Ukiwa ugenini usinyamaze sana. Wenyeji wanaweza wakadhani unafikiria kuwaua. 7. Kila mtu anauogopa usiku. Kichaa mmoja alisikika akisema, “Usiku umeingia waniroge tena.” 8. Pombe mbaya, nimekutana na mlevi anatafuta wanawake wembamba atengeneze fagio. 9. Niliwahi kupanda basi, dereva analalamika njia nzima, “Nimefanya kazi miaka mingi, mafanikio hakuna. Sasa leo mwisho.” Abiria wakaanza kuomba kushuka mmojammoja. 10. Mchana hupati hela, usiku hupati usingizi. Kwa kifupi...