Jinsi ya Kuandika Barua ya Kirafiki

Mwanaume akiandika barua katika laptop.


SHULE YA SEKONDARI SAMATA,
S. L.P 700,
DAR ES SALAAM.
09/07/2018.
Mpendwa rafiki,
Habari yako, natumaini unaendelea vyema huko nyumbani Makete. Mimi pia ni mzima wa afya.
Madhumuni ya kukuandikia barua hii, ni kutaka kukufahamisha juu ya maandalizi yangu ya mtihani wa kidato cha nne ambao ninakwenda kuufanya ifikapo tarehe tano Novemba.

Nimejiandaa vyema katika masomo yote na ninatumaini nitafaulu vyema. Pia, nimepitia mitihani yote ya taifa iliyopita na nimeona jinsi maswali yanavyotoka. Mbali na hayo, nimekuwa nikijipima kwa kufanya mitihani mbalimbali na matokeo yangu ni mazuri sana.
Basi rafiki naomba nikutakie kila la heri katika maisha yako hapo Makete. Nisalimie wote wanaonifahamu.
Rafiki yako,
Kijoto Bohari.

Popular posts from this blog

Notes za Kiswahili Kidato cha Pili | Form Two

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2025