Mtihani wa Kiswahili Kidato cha Nne 3 2019 | Fomati Mpya

mtu kabeba fagio
Endapo unataka kufanya mtihani huu ili usahihishwe na Mwalimu, zingatia mambo haya:
1. Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21.
4. Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
5. Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili).
Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66 (Daud Makoba)
“Kwa kuwa lengo la mtihani huu ni kutaka kujua uwezo na mapungufu ya mwanafunzi ili aweze kupewa mbinu mbadala za kumsaidia kufaulu mtihani wake wa mwisho, kufanya udanganyifu hakuna faida yoyote kwani lengo la mtihani si kubaini nani atakuwa wa kwanza na yupi atakuwa wa mwisho!”
It is far more honorable to fail than to cheat.
Sasa fanya mtihani wako…

Muda saa 3:00

Sehemu A (Alama 15)

1. Soma habari kisha jibu maswali yanayofuata kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.
Niliwaona masikini wakicheka. Kicheko cha ndanindani, mdomo wote kufunguka, hewa nyingi kuingia,jino la mwisho kuonekana na mbavu kidogo kubana. Walicheka kwa furaha kabwela wale. Sifahamu ni kipi hasa kiliwafurahisha.
Niliwachunguza vyema, hawakuwa na hofu. Hofu itoke wapi? Masikini hafilisiki! wa kwanza aliitwa Ntejo - Masikini. Wa pili aliitwa Mutu - Masikini, na watatu aliitwa Salamba - Masikini. Japo nilikuwa nawahi katika shughuli zangu, sikuweza kuendelea, nilisimama nikabaki nikiwashangaa.
Kumbe walikuwa katika kikao, kikacho nyeti cha kuuondoa umasikini, pengine ndiyo sababu ya kile kicheko chao kilichonivutia. Kicheko cha kukunja mbavu. Nilimsikia Ntejo akisema, “kama tukichapa kazi kwa bidii, umasikini utatoka, tutakuwa watu wengine kabisa.”
Mutu akaunga mkono, “nakubaliana nawe Ntejo, kazi ndiyo imemfanya mwanadamu mwenyewe, hakuna namna ila kuchapa kazi. Hata hivyo naomba niongezee jambo moja, tukumbuke kuweka akiba!”
Salamba akadakia, “kweli kabisa, ni lazima kuweka akiba ili isaidie wakati wa dharura, lakini pia, ikiwa kubwa, inaweza ikawekezwa na kuleta matunda mazuri zaidi. Nami nina jambo la nyongeza, elimu ya kufanya mambo inahitajika. Bila elimu ya kufanya mambo, hatutayaonja matunda ya kazi yetu ngumu.”
Masikini wale walimaliza mazungumzo, nami bado nawatazama tu, lakini wao hawanioni, raha iliyoje! Kwisha kumaliza kuzungumza, wakala kiapo kuyafanyia kazi waliyosema. Mimi nikaondoka zangu.
Baada ya mwaka mmoja, nilikutana nao tena. Wako vilevile, hawana kitu. Salamba kabeba chupa ya gongo, Mutu kashika kikombe kidogo naye Ntejo kabeba redio kubwa, wote wanacheza na kucheka kwa furaha. Nilitamani kuwachapa kofi ili kuwakumbusha waliyopanga mwaka mmoja nyuma. Lakini, Mwalimu Makoba mimi, ugomvi na walevi siuwezi. Nikaondoka zangu. Mimi na mwili wangu.
I. Kipi kinafaa kuwa kichwa cha habari uliyosoma?
A. Masikini wenye bahati b. Matajiri watatu c. Sinema zetu d. Masikini watatu
ii. Ni yapi yalikuwa majina ya masikini hao watatu?
A. Ntejo, Salamba na Musa b. Salamba, Ntejo na Yahaya c. Salamba, Ntejo na Mutu d. Mutu, salamba na Musa
iii. Kwa nini masikini wale watatu walishindwa kutimiza mipango yao?
A. Ulevi b. miundombinu duni c. walivamiwa na majambazi d. waliugua
iv. Msemo upi unaendana na kukosa hofu kwa masikini wale watatu?
A. Masikini hafilisiki b. hofu haizuii furaha c. furahi kwa afya yako d. hofu hupotea taratibu
v. Ni sentensi ipi siyo kweli kuhusu masikini hao watatu
A. Masikini walikuwa na furaha b. hawakutimiza mambo waliyopanga c. hawakuwahi kunywa pombe d. walitembea na redio
2. Oanisha sentensi za kifungu A kwa kuchagua jibu sahihi kifungu B.

kifungu A

I. Tuweke akiba.
II. Tufanye kazi kwa bidii.
III. Elimu ya kufanya mambo inahitajika.
IV. Nilitamani kuwachapa kofi ili wakumbuke waliyopanga mwaka mmoja nyuma.
V. Bila elimu ya kufanya mambo

Kifungu B

A. Lakini ugomvi na walevi siuwezi.
B. Hatutayaonja matunda ya kazi yetu ngumu.
C. Salamba
D. Ntejo

E. Mutu

Sehemu B (alama 40)

3. Bainisha njia tatu za kuambatanisha maneno ili kuzalisha maneno mapya kisha toa mifano miwili kwa kila njia uliyobainisha. (Alama 4)
4. Toa maana nne tofauti za neno “kibao” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana uliyotoa. (Alama 4)
5. Fafanua dhana zifuatazo na kisha toa mfano mmoja kwa kila dhana uliyofafanua. (Alama 8)
A. Neno
B. Kirai
C. Kishazi
6. Nyambua maneno yafuatayo ili kupata maneno mawili zaidi kwa kila neno.
A. Beba
B. Pokea
C. Rudi
D. Soma
7. Andika insha ya kisanaa isiyozidi maneno 250 kuhusu kichwa cha habari kisemacho, YALIYOWAKUTA MSITUNI. (Alama 8)
8. Kwa kutumia hoja tano, eleza mchango wa Wajerumani katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili. (Alama 8)

Sehemu C (Alama 45)

Jibu maswali matatu.
9. Fasihi simulizi ni pana na ina vitu vingi ndani yake. Ukitumia mifano, bainisha tanzu nne za fasihi simulizi.
10. “Washairi hutumia mashairi yao kuelimisha jamii kuhusu mambo yanayoikabili.” thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutumia hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili zilizoorodheshwa.
11. “Mwanamke ni mtu mwenye huruma.” Thibitisha kauli hiyo kwa kutoa hoja tatu kutoka katika vitabu viwili vya riwaya vilivyoorodheshwa.
12. “Waandishi wa tamthiliya ni mafundi wa kupotosha jamii.” kanusha kauli hiyo kwa kutumia tamthiliya mbili kati ya zilizoorodheshwa. Tumia hoja tatu kwa kila kitabu.

Majibu ya mtihani huu yanapatikana kwa sh. 1,000 (Elfu Moja) bofya hapa kuwasiliana na Mwalimu.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Notes za Kiswahili Kidato cha Pili | Form Two

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2025