Mtihani wa Kiswahili 1 Kidato cha Sita 2020 2 Fomati Mpya
Maelekezo ya Kufanya Mtihani Ili Usahihishwe na Mwalimu:
1.
Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2.
Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3.
Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya
Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21.
4.
Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
5.
Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili).
Namba
za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66
(Daud Mhuli).
Muda: Saa Tatu
Sehemu A (Alama 40)
1.
Soma
kwa makini kifungu hiki cha habari kisha jibu maswali yanayofuata:
Bwana Mako alinyanyuka katika sofa, akarusha
mateke na ngumi mfululizo mpaka alipohisi yupo sawa kwa mapambano. Mwenye
uchungu na nchi yake, alikisogeza pembeni kitanda, kisha akafunua chini katika
sakafu, humo alificha siraha zake nyingi za maangamizi. Aliamua kuchukua siraha
mojawapo, bunduki ya kisasa, Norinco 97, akaifuta vumbi na kuirudisha pahala
pake. Alipomaliza ukaguzi wa siraha, akapanga kila kitu kama kilivyokuwa awali,
kisha akachukua simu yake na kumwandikia ujumbe mfupi Lightness, “kazi
imeanza.”
Nchi ya Andalasu ilikuwa katika shida kubwa.
Mgodi pekee uliotegemewa na taifa hili masikini, ulivamiwa na kundi la
wanyang’anyi waliokuwa na siraha
za moto. Haikufahamika ni
nani alikuwa nyuma ya kundi hili. Kwa kuwa mgodi huu unaotoa Almasi kwa wingi
kuliko mgodi wowote ule Duniani ulikuwa mikononi mwa wanyang’anyi, serikali
ilipoteza fedha nyingi na ilianza kushindwa kujiendesha, hali ilikuwa mbaya
katika serikali na uchumi wa nchi nzima.
Mgodi ulipotekwa mara ya kwanza, kilitumwa
kikosi cha askari kwenda kuukomboa, askari wote waliuawa. Baada ya hapo
kikatumwa kikosi cha makomando, ambacho nacho kilifyekelewa mbali na hakuna
aliyebaki. Vikosi vingi viliendelea kutumwa na matokeo yalikuwa yaleyale,
hakuna aliyerudi akiwa hai. Serikali ikawa katika hofu kubwa ya wanyang’anyi
hawa wasiofahamika.
Vikosi vingine vilipotumwa kwenda kupambana
na wanyang’anyi hawa, vilikataa kwa kutoa sababu kuwa, silaha walizotumia wao
zilikuwa za kiwango cha chini mno ukilinganisha na wanyang’anyi ambao wao
walitumia silaha kali zaidi. Wakati askari wa serikali wakienda kuvamia wakiwa
na siraha aina ya SMG yenye uwezo wa kubeba risasi 30, wanyang’anyi walitumia
siraha za maangamizi kama IWI X95 TAVOR ambayo iliweza kupiga risasi 950 kwa dakika! Mwenye nguvu
mpishe!
Maswali
a.
Andika
kichwa cha habari hii kwa maneno yasiyozidi matatu.
b.
Toa
maana ya maneno haya kama yalivyotumika:
i.
Sofa
ii.
Siraha
iii.
Mgodi
iv.
Wanyang’anyi
v.
Askari
c.
Usemi,
‘mwenye nguvu mpishe, una maana gani?’
d.
Taja
funzo moja ulilolipata katika habari hiyo.
2.
Eleza
faida tano za kujifunza sarufi ya Kiswahili.
3.
kwa
kutumia mifano, eleza maana ya istilahi zifuatazo:
i.
mofimu
ii.
mofimu
huru
iii.
viambishi
iv.
mzizi
4.
huku
ukitoa mifano, taja mitindo mitano ya lugha kutokana na mazingira.
Sehemu B (Alama 60)
Jibu maswali matatu,
swali la 8 ni la lazima
5.
Andika
insha ya hoja kuhusu mada isemayo, ‘Faida za mazoezi.’
6.
Kwa kutumia hoja sita, tathmini hoja zinazodai
kwamba kiswahili ni kiarabu, pijini au kreoli.
7. Fafanua
maana na matumizi ya lugha ya kwanza, pili, rasmi na lugha ya taifa.
8. Tafsiri
matini hii ya Kiingereza, kuwa katika lugha ya Kiswahili:
I’m told that there once was
a stranger from some other town who was walking in a plantation along the
coast. As he walked along, he suddenly saw a very pretty little necklace lying
on the road. He snatched up the necklace and threw it into his mouth because
there was another person walking behind him and he didn’t want him to see the
necklace. The necklace was really a snake. He died immediately. He died because
he didn’t realize that it was a snake; he didn’t know he put a snake into his
mouth rather than a necklace.