Mtihani wa Kiswahili Kidato cha Tatu 2020 1
Maelekezo ya Kufanya Mtihani Ili Usahihishwe na Mwalimu:
1.
Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2.
Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3.
Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya
Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21.
4.
Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
5.
Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili).
Namba
za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66
(Daud Mhuli).
Muda saa 2
Jibu
maswali yote
Sehemu A (Alama 15)
1.
Chagua herufi ya jibu sahihi kutoka katika
kipengele I hadi V, kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu cha
kujibia.
i.
Ni ipi maana ya ngeli?
A. Ni
upangiliaji wa nomino katika makundi yanayofanana B. Ni mfumo ambao majina yote
hupewa kipaumbele na hadhi ya kuwa vitenzi C. ni ubadilishaji wa nomino kuwa
vivumishi D. Ni neno lenye asili ya kihaya likiwa na maana ya kunyumbulisha.
ii.
Sentensi ipi kati ya hizi haijazingatia upatanishi
wa kisarufi?
A. Mtoto
anacheza uwanjani B. baba wanalima shamba C. rais ana hutubia mkutano D. watoto
amelala chumbani
iii.
Huu ni mfano wa kirai nomino
A. Mtoto
yule B. yule mzee C. kwa baba D. Piga mjomba
iv.
Huu ni mfano wa kishazi tegemezi.
A. Samaki
mkunje angali mbichi B. mtoto ameokolewa C. shamba limenunuliwa D. mbuzi
aliyekuwa mgonjwa
v.
Huu ni mfano wa sentensi ambatano
A. Mama
anapika chakula B. mtoto aliyelala ameamka C. mama anapika na baba anafua D.
Hamis angelijua angenilipa pesa zangu.
Sehemu B (alama 40)
2.
Eleza kwa ufupi kuhusu madai haya:
i.
Kiswahili ni kiarabu
ii.
Kiswahili ni pijini au kreoli
iii.
Kiswahili ni kikongo
iv.
Kiswahili ni kibantu
3.
Toa mifano minne ya ushahidi wa kimsamiati
unaothibitisha kuwa Kiswahili ni Kibantu.
4.
Toa mifano minne ya ushahidi wa kimuundo
inayothibitisha kuwa Kiswahili ni kibantu.
Sehemu C (alama 45)
5.
Kwa kutumia mifano, bila kujali mpangilio
wake, fafanua aina sita za ngeli kwa kuzingatia kigezo cha upatanisho wa
kisarufi.
6.
Eleza aina tano za virai.
7.
Jadili aina tatu za sentensi huku ukitoa
mifano mitatu kwa kila aina ya sentensi.