Mambo Muhimu ya Kumfundisha Mtoto Yeyote
1.
Watu
wakikuuliza unataka kuwa nani ukiwa mkubwa, wajibu huna mpango wa kuwa mkubwa
Waambie
utaamua ukikua. Waeleze kuwa mkubwa kuna tisha kama kuzimu, usiogope, waeleze.
2.
Kuwa
makini na mapenzi na yule unayempenda kwanza
Mama,
dada, kaka, baba na ndugu zako wengine, wanachukua nafasi ya pili. Nafasi ya
kwanza ni wewe mwenyewe.
3.
Jifunze
kuwa mbunifu, siyo mshindani
Ushindani
unatumia nguvu nyingi na pesa kuliko ubunifu. Thamani ipo katika ubunifu na
siyo ushindani.
4.
Kuwa
na marafiki bila kujali rangi, kabila wala dini
Elewa
kwamba, wanaowabagua wengine ni wajinga na kamwe hawapaswi kuigwa.
5.
Usiamini
kila unachosikia
Chunguza
ubaini mwenyewe. Usikubali kila kitu, vingine ni uongo uliotungwa na waongo wa
dunia.
6.
Usiende
shule ili uajiliwe kazi nzuri, nenda shule ili uwe tajiri
Mfumo
wa sasa, utakufanya uajiliwe na bosi ambaye alishindwa mtihani ambao wewe
umefaulu. Elimu binafsi itakufanya tajiri.
7.
Tafuta
maarifa
Maarifa
ni kitu cha lazima, kuna faida gani ya kuwa na mali, kisha ukaipoteza mali hiyo
kwa sababu ya kukosa maarifa?
8. Waheshimu
wazazi wako
Jinsi
unavyowafanyia wazazi wako, watoto wako watakufanyia hivyo hivyo. Ukiwafanyia ubaya,
na wao watakufanyia ubaya. Ukiwa mwema, nao watakuwa wema kwako.
9.
Furahia
maisha na usiruke hatua
Hatua
ya maisha utakayoiruka, utaifidia uzeeni. Itashangaza ukililia kubebwa mgongoni
uzeeni.