Kanuni Kumi za Maisha Ambazo Hazisemwi Sana
1. Mtu akikuonesha picha moja katika simu
yake, usiweke picha nyingine
Pia
usimwombe ruhusa ya kutazama picha zingine, ishia hiyo moja labda aamue
kukuonesha picha zingine kwa hiyari yake.
2.
Kabla
hujafanya kazi yoyote, kakojoe kwanza
Haijalishi
ni kazi gani, nenda kajiweke sawa. Ipo siku utanishukuru kwa ushauri huu.
3.
Ukiazima
gari, irejeshe ikiwa imejaa mafuta
Hii itamfanya
aliyekuazima ajivunie kukuazima. Lakini, itampunguzia hasara aliyoingia wakati
anakuazima gari lake, pengine wakati anakuazima gari hilo lilikuwa na mafuta. Ni
dalili njema kurejesha gari likiwa limejaa mafuta.
4.
Usiweke
mziki kwa sauti kubwa ukiwa katika kundi la watu
Siyo
kila mtu anataka kusikiliza unachosikiliza. Usiwe kero, tumia spika za masikio.
5.
Kuna
wakati haupo sahihi
Siyo
vibaya kukosea. Tambua kuwa umekosea, kubali na jifunze kupitia makosa yako.
6.
Usifanye
maigizo katika msiba
Wamefiwa
na mpendwa wao. Usiwakwaze tafadhali, kuwa mpole na kama huwezi kutulia, rudi
nyumbani haraka.
7.
Unapotafuna,
funga mdomo wako
Ni ajabu
kuwa, watu wengi hutafuna midomo ikiwa wazi. Siyo tabia nzuri, funga mdomo wako
kisha tafuna.
8.
Ukiazima
kitu kwa mara ya tatu, nunua chako
Ukiazima
kitu kwa mara ya tatu maana yake ni kwamba, una kihitaji sana kitu hicho. Hivyo
nunua chako, itakusaidia.
9.
Usichungulie
katika vipande vya mlango wa bafuni
Tabia
mbaya hii. Unataka kuona nini? Tafadhali, nenda zako kwa amani, usifikiri
kufanya jambo hili.
10.
Heshimu
kila mtu
Wote
ni watu, wote ni binadamu. Heshimu kila mtu bila kujali chochote, ukifanya
hivi, mafanikio ni yako.