Mada za History Zinazotoka Zaidi Katika Mtihani Kidato cha 4
Nimekuwa
nikiulizwa swali hili na wanafunzi wangu wengi. “Mwalimu ni mada gani zinapenda
kutoka katika mtihani wa History kidato cha nne?” wanaouliza swali hili wamegawanyika
katika makundi matatu:
Kundi
la kwanza ni wanafunzi wavivu, wanataka wajue mada zinazotoka katika mtihani
ili wasome hizo tu na wasihangaike kusoma mada zingine.
Kundi
la pili ni wanafunzi wanaotaka kufahamu waweke msisitizo wa kusoma mada gani zaidi.
Na kundi
la mwisho, huuliza bila kuwa na sababu maalumu, wao huuliza tu.
Nasisitiza
kuwa, siyo kosa kutaka kufahamu mada zinazotoka zaidi katika mtihani wa History kidato
cha nne.
Ni mada gani hutoka zaidi katika mtihani wa History kidato cha nne?
Mada
zote hutoka katika mtihani wa kidato cha nne. Ili uweze kufaulu mtihani wako wa
History, unashauriwa usome mada zote za kidato cha kwanza, pili, tatu na
nne, utaweza kufaulu vizuri mtihani wako.
Pia,
lengo la somo la History siyo kufanya mtihani pekee, lengo kuu ni kukupa
maarifa ya Historia yako ili utambue ulipotoka, ulipo na unapokwenda.
Baada
ya kuwa umesoma mada zote, sasa tambua ya kwamba, kuna mada zina alama nyingi zaidi
katika mtihani kwani mada hizi hupenda kutoka katika maswali ya maelezo. Mada hizo
ni:
Establishment of colonialism, Colonial administration, Colonial Economy, Colonial social services, Crises na nationalism and decolonization.
Wakati
mada zote hutoka katika mtihani wako, inawezekana mada tajwa hapo juu zikawa na
alama nyingi zaidi kuliko mada zingine.
Zingatia
kwamba hayo ni maoni yangu tu, kwani inawezekana maswali mengi ya kujieleza
yakatoka kidato cha kwanza au cha pili.
Sasa
nakuomba ufuate kile ambacho nimekuwa nikiwaeleza wanafunzi wangu ambao siku
zote hufaulu mitihani yao ya History kwa alama zenye kuacha tabasamu:
“Hakuna
mada zinazopenda kutoka katika mtihani wa History, mada zote hutoka na jambo la
msingi ni kusoma mada zote yaani, mada nne kidato cha kwanza, mada nne kidato
cha pili, mada nne kidato cha tatu na mada nne kidato cha nne.”