Ni Somo Gani Kubwa Maisha Yamekufundisha?
Nilikuwa
katika kiota cha burudani, humo nilikwenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa
rafiki yangu mmoja ambaye tumefahamiana kwa miaka dahari. Katika meza
niliyokaa, tulikaa wawili, mimi na dada mmoja ambaye hatukuwahi kuonana kabla. Hata
hivyo, haikuchukua muda kufahamiana na kuanzisha mazungumzo.
Wakati
sherehe ikiendelea, dada aliniuliza swali, “Mwalimu Makoba, ni somo gani kubwa
maisha yamekufundisha?”
Nilitafakari
kidogo, kisha nikajibu:
“Nimejifunza
kwamba hakuna njia ya mkato katika
maisha.
Watu
wenye miili mizuri isiyo na vitambi wala unene kupitiliza wanastahili. Siyo uchawi. Wamefanikiwa kwa maamuzi waliyofanya ikiwemo kupangilia mlo na kufanya mazoezi.
Watu
wenye mafanikio wanastahili. Mafanikio hayaji kwa bahati tena hayatokei kwa
usiku mmoja. Wamefanikiwa kwa sababu waliamua kufanikiwa.”
Nilimaliza
kuzungumza, nikabaki kusikiliza mziki na kusukuma mafunda kadhaa ya kinywaji
nilichopewa. Nilimsikia dada akirudia maneno niliyosema,
“HAKUNA
NJIA YA MKATO KATIKA MAISHA.”