Notes za Civics Form Three | Kidato cha Tatu
Notes
za Civics kidato cha tatu, ama kwa Kiswahili sahihi, nukuu za somo la uraia
kidato cha tatu zinahitaji umakini mkubwa katika kuziandaa kwani, vitabu vya
kurejea ni vichache.
Somo
la Civics kidato cha tatu lina jumla ya mada tatu kama kilivyo kidato chenyewe,
mada hizo ni:
Mada
ya kwanza iitwayo ‘Life Skills’ inahusu maarifa mbalimbali anayopaswa kuwa nayo
mtu ili aweze kuishi vyema katika jamii yake. Miongoni mwa maarifa yanayoelezwa
katika mada hii ni: uongozi bora, kujiamini mwenyewe na kufanya kazi kwa
kushirikiana.
Bila
shaka malengo ya mada hii, ni kumfanya mwanafunzi azidi kupata maarifa sahihi
yatakayomwezesha kuishi vyema katika jamii yake.
Mada
ya pili iitwayo ‘Economic and Social Development’ inahusu masuala ya maendeleo
ya kiuchumi na kijamii. Mada hii inamfundisha mwanafunzi maana ya maendeleo,
viashiria vya maendeleo, mambo yanayosababisha maendeleo, mchango wa serikali
katika kuleta maendeleo, mchango wa taasisi za fedha katika kuleta maendeleo na
mchango wa taasisi binafsi katika kuleta maendeleo. Pia, mada hii inaisha kwa
kuonesha mipango mbalimbali ya kujiletea maendeleo pamoja na mafanikio yake.
Mada
hii itamfanya mwanafunzi atamani kupata maendeleo yake na jamii na hatimaye
kuondokana na adha ya ukosefu wa maendeleo katika jamii yetu.
Mada
ya tatu ambayo ndiyo mada ya mwisho kwa kidato cha tatu inaitwa ‘Poverty’. Mada
hii inahusu umasikini. Katika mada hii, mwanafunzi atajifunza maana ya umasikini,
mambo yanayosababisha umasikini na jinsi ya kufanya ili kuondokana na
umasikini.
Mada
hii itawafanya wanafunzi wabadili mtazamo wao kuhusu umasikini na kuwafanya
waongeze mapambano dhidi ya umasikini na hatimaye kuiletea maendeleo jamii yetu
ya Tanzania.
Notes
hizi za Civics kidato cha tatu, zimeandaliwa kwa weledi mkubwa na Mwalimu
Makoba, zimezingatia lugha rahisi inayoeleweka kwa wasomaji Watanzania ambao
kiingereza siyo lugha yao ya kwanza.
Mwanafunzi
anaweza kusoma ‘notes’ hizi bure katika mtandao huu, lakini hata hivyo,
atatakiwa kuunga kifurushi kila atakapo kusoma. Endapo mwanafunzi angetaka awe
na ‘notes’ zake mwenyewe na asome muda wowote bila kuhitajika kuunga kifurushi
cha intaneti, anashauriwa kununua na atatumiwa katika mfumo wa PDF kokote
alipo.
Nawatakia
usomaji mwema.