Uundaji wa Maneno | Kiswahili Kidato cha Pili
Uundaji
wa maneno ni ujenzi au uzalishaji au utengenezaji wa maneno mapya. Uundaji wa
maneno mapya husaidia kuongeza msamiati katika lugha ili kukidhi mahitaji ya
mawasiliano. Uundaji wa maneno mapya husababishwa na mabadiliko ya kiuchumi,
kisiasa na kiutamaduni na maendeleo ya kisayansi yanayotokea katika jamii. Kwa
mfano tunayo maneno mapya, kama vile ufisadi, uwekezaji, ukeketaji, ujasiriamali
na mengine mengi kutokana na mabadiliko ya kijamii.
Uambishaji ni nini?
Uambishaji
wa maneno ni kitendo cha kupata maneno kwa kubandika Mofimu kwenye kiini cha
neno. Uambishaji hutokea kabla ya kiini cha neno au mzizi wa neno. Mfano kiini
pig- unaweza kuunda maneno kama inapiga, anayepiga, mpigaji, amepigika nk.
Mofimu
zinazopachikwa katika mizizi huitwa Viambishi.
Aina za uambishi
Kuna
aina mbili za viambishi;
Viambishi awali:
Hivi ni viambishi vinavyo pachikwa kabla ya kiini/mzizi wa kitenzi. Kwa mfano anaimba,
viambishi awali vya kitenzi anaimba -imba- ni a- na-
Viambishi tamati: Hivi ni viambishi vinavyopachikwa baada ya kiini/mzizi
wa kitenzi. Kwa mfano kitenzi anacheza, kiambishi tamati ni a- inayotokea baada
ya z-
Dhima za Mofimu
Mofimu
ni neno au sehemu ya neno inayobeba maana maalumu ambayo ikigawanywa katika
vipande zaidi hupoteza maana. Maneno haya ni mofimu: mama, punda, wali, bunge,
huru, na, ta, li, na kalamu.
Aina za mofimu
1. Mofimu huru
Ni
aina ya mofimu ambayo herufi zinazoiunda huleta maana kamili. Mfano: baba,
mama, shangazi, amini, imani, wewe, redio na bendera.
Mofimu tegemezi
Ni
aina ya mofimu ambayo herufi zinazoiunda hazileti maana kamili. Mfano: li, na,
pik.
Zifuatazo ni dhima za mofimu:
1. Huonesha nafsi
Mfano:
katika neno ninacheza, mofimu ‘ni’ inaonesha nafsi ya kwanza umoja.
2. Huonesha njeo (muda)
Mfano:
katika neno alikuja, mofimu ‘li’ inaonesha wakati uliopita.
3. Huonesha urejeshi
Mfano:
waliolala, mofimu ‘o’ inaonesha urejeshi wa watenda.
4. Huonesha ukanushi
Mfano:
sikucheza, mofimu ‘si’ inaonesha ukanushi.
Mnyambuliko
Mnyambuliko
ni namna ya kuunda neno jipya kwa kutumia neno la awali kwa njia ya kulirefusha
zaidi.
Mifano:
Habari
- habarisha
Sasa
- sasisha
Piga
- pigisha
Mazingira yanayosababisha mahitaji ya maneno mapya
Yapo
mazingira yanayosababisha kuwe na uhitaji wa kupata maneno mapya. Mazingira
hayo ni:
1. Sayansi na teknolojia
Kukua
kwa sayansi na teknolojia ni sababu ya uhitaji wa maneno mapya. Hivyo mpaka
sasa tuna maneno mapya ya sayansi na teknolojia. Maneno hayo ni kama: tarakilishi,
luninga n.k
2. Elimu
Katika
elimu kunahitajika maneno mapya kila siku. Kwa mfano, katika taaluma kuna
tafiti na gunduzi mbalimbali hivyo, maneno mapya kwa ajili ya vitu
vilivyogunduliwa huhitajika.
3. Uandishi wa habari
Waandishi
wa habari wanahitaji maneno mapya ili waweze kuendana na kazi yao. Neno
mubashara, limepatikana katika mazingira haya.
Dhima ya mnyambuliko wa maneno
1. Kurefusha maneno
Mfano:
piga, pigia, pigiwa, pigika
Cheza,
chezewa, chezeka.
2. Kuongeza maneno
Mfano:
bora, boresha, boreshewa.
3. Kupanua maana ya maneno
Mfano:
Piga
- kukutanisha vitu kwa nguvu.
Pigia
- piga kwa sababu fulani.
4. Huzalisha kauli mbalimbali
Mfano:
Piga
- kauli ya kutenda.
Pigiwa
- kauli ya kutendewa.
Maswali
1. Eleza maana ya viambishi awali huku
ukitoa mifano.
2. Eleza kazi tano za viambishi awali
huku ukitoa mifano.
3. Onyesha viambishi awali vilivyomo
katika maneno yafuatayo, kisha ueleze shina la kila kimoja:
A. Mlezi B. Tuliompinga C. Wanajivisha D.
Hajasoma E. Umeshiba F. Amefika
4. Eleza maana ya uambishaji.
5. Fafanua dhima ya uambishaji katika
lugha.
6. Nini maana ya viambishi?
7. Onyesha namna uambishaji unavyotokea
katika aina mbalimbali za maneno.
8. Eleza kazi nne za mnyambuliko katika
lugha ya Kiswahili.
9. Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kaul
nne kila moja:
A. Omba B. Shawishi C. danganya D. Unga
10. Eleza maana ya jozi za maneno
yafuatayo:
A. Enea, eneza B. Changanya,
Changanyikiwa C. Angua, angusha D. Someka, somesha E. Tengewa, tengana
11. Geuza kauli zifuatazo katika kauli
tendana:
A. Mwalimu alimsaidia mzazi kubeba mzigo.
B. Amani itatokea tu ikiwa wanachi watawaamini
viongozi.
C. Mwanachama ameamua kumshika mkono
mwenzake baada ya ushindi.
D. Ni kweli kwamba, Ria atamshinda Ari
kesho.
E. Mshtaki ameafiki mshitakiwa alipe
faini.
F. Tunga sentensi yenye vitenzi
vifuatavyo:
A. Gombana B. Rudiana C. Andikiana D.
Tabiriana E. Ridhiana F. peana