Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Vifaa ya kuandikia CV
Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi.

CV au wasifu ni kitu cha lazima kwa yeyote anayeomba kazi. Watu wengi wanaokosa kazi, tatizo huwa siyo wao, bali tatizo huwa ni CV zao. Kumekuwa na makosa mengi katika uandishi wa CV jambo ambalo limesababisha watafuta kazi wengi kushindwa kuitwa kwenye usaili.


Makala hii itakueleza namna sahihi ya kuandika CV, utaitwa katika ‘interview’ nyingi endapo utaandika CV sahihi. Tena nakukumbusha, kila taaluma ina aina yake ya CV, CV ya rubani haifanani na CV ya injinia. Vivyo hivyo, CV ya mpishi haifananani na CV ya Mwalimu.

Pia nakukumbusha usome jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi, kwani CV huenda pamoja na barua ya maombi ya kazi.

CV Bora ni Ipi? Ukurasa Mmoja au Kurasa mbili hadi tatu?

CV bora ni ile yenye kurasa mbili hadi tatu. Watu wengi wanapojifunza namna ya kuandika CV, wamekuwa wakiona CV zenye ukurasa mmoja, picha nzuri na zimepambwa kwa rangi nyingi. nao hutamani kuwa na CV za aina hiyo. Ieleweke kwamba, kila nchi ina utaratibu wake inaofuata katika masuala ya uandishi. Nyingi ya CV hizo zinawahusu hasa watu kutoka Ulaya. Mfumo mzuri na unaokubalika katika nchi yetu ni ule wa CV inayoanzia kurasa mbili na kuishia kurasa tatu. CV yenye ukurasa mmoja haitoshi kuonesha mambo yako kwa nafasi na inawaeleza waajiri wako kuwa huna uzoefu wa kutosha.

Andika CV yako, siyo lazima kuweka picha, lakini kama unataka basi iweke upande wa juu kushoto. Kama CV yako inapokelewa kama nakala ngumu, bandika picha ya 'passport' upande wa juu kulia.

CV Hatua kwa Hatua

Hatua ya kwanza nitaonesha mfano wa CV kwa lugha ya Kiswahili na hatua ya pili nitaonesha mfano wa CV kwa lugha ya Kiingereza halafu utachagua mwenyewe utumie lugha gani katika kuandika CV yako.

CV ya kwanza, ni CV ya kawaida, ni aina hii ya CV utaikuta katika vitabu mbalimbali na hufundishiwa wanafunzi:

Mfano wa Kwanza: CV ya Kiswahili ambayo ni ya kawaida

WASIFU WA SAMWEL MANATI MALUMBAGA
Taarifa za Awali
Jina: Samwel Manati Malumbaga
Ndoa: Ameoa
Barua Pepe: samwelimbaga@gmail.com
Simu: 0754 89 53 21
Utaifa: Mtanzania
Tarehe ya kuzaliwa: 02/08/1986
Historia ya Elimu
2007-2008, VETA Dodoma.
2013-2016, Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege. Cheti cha Kidato cha Nne.
19966-2012, Shule ya Msingi Makole. Cheti cha Darasa la Saba.

Uzoefu
2012-2013, Mgodi wa Bulyanhulu.
Maarifa
- Kutumia Kompyuta.

Ninapenda
Kufanya kazi, Kufundisha, Kusoma, Kujifunza mambo mapya.

Wadhamini:
1. Mwalimu Makoba
Barua Pepe: daudmakoba@rocketmail.com
Contact: 0754 89 53 21
Dar es Salaam.

2. David Mwakimonga,
Mkufunzi,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
S.L.P 35040,
Dar es Salaam.

Mfano wa Pili ni mfano wa CV iliyo katika lugha ya Kiingereza, lakini CV hii ni ya kawaida.

Mfano wa Pili: CV ya kiingereza ya Kawaida


CURRICULUM VITAE OF MATIKO PANDAMELI
Particulars
Name: Matiko Pandameli
Marital status: Single
E-mail: matiko@gmail.com
Telephone: 0653 250 566
Nationality: Tanzanian
Date of birth: 14/10/1996

PROFILE
I am a creative, influential, corporative and enthusiastic person with well-organized performance, intellectual and competence in the areas of health.
Academic Background
Duration
Institute attended
Award
2017-2019
Rukwa College of Health and Allied Sciences
Diploma in Medical Attendant
2015-2017 Bagamoyo Secondary School Advanced Certificate of Secondary Education (ACSE)
2011-2014 Nkasi Secondary School Certificate of Secondary Education(CSE)
2004-2010
Namanyere Primary SchoolCertificate of Primary Education

Work experience
Place: Nazareti Dispensary in Mbozi Songwe
Position: Medical attendant
Date: October 2014 – January 2015
Place: Matai Dispensary in Karambo Rukwa
Position: Medical Attendant
Date: March 2016 - May2016
Language Proficiency
Swahili: Excellent written and oral skills.
English: Excellent written and oral skills.
Skills
- Presentation and teaching skills.
- Communication skills.
- Good interpersonal skills.
- Computer literate: competent in MS Word, MS Excel, MS Publisher, MS PowerPoint.

Interests
Teaching, social networks, creative writing, music, reading books, football, swimming, playing game.
Referee available on request
Mwalimu Makoba,
Mwalimu Makoba Open School,
Email: daudmakoba@rockemail.com,
Contact: 0754 89 53 21,
Dar es Salaam.

Mr. David Mwakimonga,
Assistant Lecturer,
University of Dar es Salaam,
P. O. Box 35040,
Dar es Salaam.

Mr. Jonathan Tangwa,
Principal of IEDS,
P.O.Box 7775,
Dar es Salaam.
Declaration
I, SAMWELI MANATI MALUMBAGA, do hereby declare and state that, the information given on this curriculum vitae is true to the best of my knowledge.

Mfano wa Tatu: CV ya Kiingereza Iliyoandikwa Kitaalamu Zaidi

Mfano huu ni wa CV ya kitaalamu zaidi. Kazi zote nilizowahi kuomba, niliandaa CV yangu katika mfumo huu na mara zote niliitwa katika interview. Watu wengi niliowahi kuwaandikia CV na ninaoendelea kuwaandikia CV nimekuwa nikitumia mfumo huu unaokubalika kwa waajiri wote, yaani binafsi na serikali. Tazama mfano wake:
Mfano wa CV ya Kiingereza 1

Mfano wa CV ya Kiingereza 2

Mfano wa CV ya Kiingereza 3
Mfano wa Nne: CV ya Mwalimu-Kiingereza
Cv ikionyesha taarifa za awali


CV ikionyesha umahiri wa lugha








CV ikionyesha historia ya masomo

CV ikionyesha uzoefu wa kazi

CV ikionyesha maarifa


Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi.

Popular posts from this blog

Notes za Kiswahili Kidato cha Pili | Form Two

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2025