Namna Sahihi ya Kusoma Itakayomsaidia Mwanafunzi Kufaulu
Wanafunzi
wenzako wanasoma kidogo, lakini wanafaulu vizuri. Wewe unakesha darasani, huna
muda wa kupumzika, lakini matokeo yako ni mabaya! Tatizo lipo katika namna
unavyosoma. Hata ukikesha, hutaweza kufaulu endapo hutakuwa na namna sahihi ya
usomaji.
Hizi
ni mbinu sahihi za usomaji ambazo zitakusaidia uweze kufaulu mitihani yako:
1.
Weka
malengo
Usisome
bila malengo. Lazima kuwe na sababu ya wewe kusoma. Miongoni mwa sababu za
kusoma zinaweza kuwa: kufaulu mtihani, kumaliza shule au chuo, kupata alama
nzuri, kuwafurahisha wazazi na wewe mwenyewe ama kupata ujuzi kwa ajili ya kazi
utakayofanya siku zijazo.
2.
Chagua
sehemu sahihi ya kusomea
Unashauriwa
kuchagua sehemu ambayo ina mwanga wa kutosha na ambayo haina makelele. Wapo wanafunzi
ambao wanapenda kusoma katika sehemu zenye kelele, kama una uwezo huo siyo
vibaya. Hata hivyo ushauri wangu ni kuwa, sehemu isiyo na kelele nyingi ni
nzuri zaidi kwa kusoma.
3.
Epuka
vitu vitakavyokuzuia kusoma
Kusoma
ukiwa unasikiliza redio au unaangalia televisheni kutakufanya uache kusoma kwa
muda na umakinikie kusikiliza au kutazama kitu fulani kitakachokufurahisha. Vivyo
hivyo kusoma ukiwa na simu yako huku ukipokea simu na kujibu meseji Haifai. Ukiamua
kusoma, hakikisha kazi inakua moja tu. Kusoma.
4.
Penda
kusoma
Usisome
kwa kujilazimisha. Usisome kwa sababu ni muda wa kusoma na usipofanya hivyo
utafokewa. Penda kusoma, tambua kwamba, elimu unayoipata hapo ndiyo maisha yako
ya baadae.
5.
Tumia
muda vizuri
Usiwe
mtu wa kuahirisha mambo. Panga ratiba na ifuate. Pia, orodhesha mambo yote unayotaka
kuyafanya katika siku fulani kisha hakikisha yote unayafanya na kuyakamilisha.
Usiwe mtu wa kukamilisha mambo kesho, kamilisha mambo leo.
6.
Usiwe
na hofu ya mtihani
Ili usiwe
na hofu ya mtihani, jiandae mapema. Kadri maandalizi ya mtihani yalivyomazuri,
ndiyo hofu ya mtihani inavyozidi kupungua. Pia, katika mtihani, usijilinganishe
na wengine. Usifikirie, “Makubi atapata alama nyingi kuliko mimi.” Wala, “sijui
kitu kabisa, mtihani huu nakwenda kufeli.”
Epuka
mawazo hasi, fikria mawazo chanya pekee. Weka mawazo haya unaposoma, “nakwenda
kufaulu mtihani huu kwa sababu nimejiandaa vizuri.”