Notes za History Form One | Kidato cha Kwanza
Notes za History kidato cha kwanza ni:
Sources and importance of history ni mada ambayo inazungumzia vyanzo mbalimbali
tunavyoweza kuvitumia ili kupata historia ya mahali fulani. Vyanzo hivyo ni
kama: masimulizi ya mdomo, makumbusho na masalia ya viumbe wa kale. Pia, mada
hii inaeleza faida za kusoma somo la Historia.
Evolution of man, technology and environment ni mada ambayo inahusu jinsi mwanadamu
alivyobadilika kutoka umbo lililofanana na nyani, mpaka alivyo leo hii. Pia,
mada hii inagusia suala la mabadiliko ya kiteknolojia kutoka matumizi ya dhana
za mawe mpaka kufikia kutumia dhana za chuma na teknolojia nyinginezo.
Development of economic activities and their impact ni mada inayozungumzia maendeleo ya
shughuli za kiuchumi kama kilimo na biashara. Mada hii imejadili kwa kina jinsi
jamii za kiafrika zilivyokuwa zikiendesha uchumi wake.
Development of social and political system ni mada ambayo inahusu jinsi jamii za kiafrika
zilivyokuwa zinajiongoza. Zipo jamii ambazo zilikuwa zinajiongoza katika mifumo
ya ukoo, na zipo jamii ambazo zilifikia hatua ya kua na wafalme wake wenyewe.
Jamii ambazo zilijitawala kwa kuzingatia umri na jinsia, hazijasahaulika katika
mada hii.
Mada
hizo nne za history kidato cha kwanza, zinatakiwa zisomwe kwa makini na
mwanafunzi ili aweze kupata mambo ambayo yamelengwa. Mbali na kuweza kufaulu
mtihani wake, mwanafunzi atapata maarifa yatakayomsaidia katika jamii yake
endapo tu, atazielewa kwa kina mada hizo.
Pia,
mwanafunzi anashauriwa afanye maswali ya kujipima ambayo yapo mwishoni mwa kila
mada. Maswali hayo ndiyo yatampa uhakika kama anaelewa anachokisoma au haelewi.
Notes
hizi, zimetumia lugha rahisi ambayo wanafunzi wengi wanaweza kuimudu na
kuelewa. Hivyo ni matumaini yangu kuwa, notes hizi zinakwenda kuwa msaada
mkubwa kwa wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na walimu.