Tabia 11 za Usomaji Zitakazokupatia Matokeo Mazuri
Unaposoma,
lengo huwa ni kupata alama nzuri zitakazokusaidia kutimiza yale uliyopanga. Inawezekana
unataka kupata A, B, C na wapo wanafunzi wanaotaka kupata D. Ili uweze kupata
alama nzuri unazohitaji wewe, zingatia tabia hizi za usomaji:
1.
Tengeneza
ratiba
Unapokuwa
unasoma, kuwa na ratiba ya wiki nzima. Ratiba itakusaidia kuwa makini katika
masomo na kuepuka kupoteza muda.
2.
Soma
kadri ya uwezo wako
Tumia
muda wako mwingi kusoma. Hii haina maana kwamba hutakiwi kupumzika, ila kusoma
kiwe kipaumbele.
3.
Vuta
pumzi ndefu kabla hujaanza kusoma
Kuvuta
pumzi ndefu kabla hujaanza kusoma hukusaidia uwe makini katika unachokisoma na
kuepusha mawazo mengine. Unapokaa kuanza kusoma, vuta pumzi ndani kwa pua,
kisha itoe kwa njia ya mdomo. Wakati ukivuta pumzi, hesabu sekunde nne, na
wakati unaitoa, hesabu sekunde nne. Itakusaidia ku’concentrate’ wakati wote
utakaotumia kusoma.
4.
Kuwa
na sababu inayokufanya usome
Usisome
kwa sababu watu wote wanasoma. Tafuta sababu ya kufanya hivyo: wengine husoma
ili waweze kupata vyeti, kupanda vyeo, kupata kazi, kupata maarifa na sababu
nyinginezo. Wewe pia, tafuta sababu inayokufanya usome.
5.
Nukuu
unapokuwa darasani
Usisikilize
peke yake, nukuu yale yanayofundishwa na mwalimu. Huwezi kukumbuka mambo yote
yanayosemwa na mwalimu, hivyo nukuu.
6.
Yasome
yote uliyofundishwa shuleni katika siku husika
Kama
shuleni ulifundishwa Kiswahili, History na Physics au masomo yoyote, yapitie
masomo hayo kabla hujaendelea na ratiba yako. Hii itakusaidia uelewe vizuri
kwani bado utakuwa na kumbukumbu juu ya kile ulichofundishwa. Usisubiri mambo
yawe mengi ndiyo uanze kusoma.
7.
Soma
‘notes’ zako kabla hujafanya maswali uliyopewa
Kabla
hujajibu maswali ya mwalimu, soma kwanza nukuu zako. Itaifanya akili yako iwe
tayari kujibu maswali hayo.
8.
Lala
kwa muda wa kutosha
Ni
vizuri zaidi kama utapata saa nane za kulala kila siku. Hata hivyo, kama mambo
ni mengi, hakikisha angalau unalala kwa saa saba au sita.
9.
Pata
mazingira mazuri ya kusoma
Sehemu
ambayo haina kelele wala usumbufu wa aina yoyote, ni nzuri kwa kusoma. Epuka sehemu
zenye makelele na vikwazo vingine vitakavyokukatisha wakati ukisoma.
10.
Pumzika
Usisome
mfululizo, pumzika. Wakati unasoma, kuwa na saa pembeni. Kila baada ya dakika ishirini,
pumzika kwa muda wa dakika moja: simama, tembea kidogo, jinyooshe, vuta pumzi
ndefu kama nilivyoelekeza, kisha endelea tena kusoma.
11.
Jipime
mwenyewe
Usisubiri
mtihani wa mwalimu ndiyo ujipime maarifa yako. Tafuta maswali katika vitabu au
mtihani wowote wa online, kisha fanya ili uone uwezo ulionao katika somo
husika. Hii itakusaidia kutambua mapema uwezo wako na kuchukua hatua
zitakazokusaidia.
Anza
leo kufanya mambo hayo, utaona mafanikio.