Ngeli za Nomino | Kiswahili Kidato cha Tatu
Ngeli
huweza kuainishwa kwa vigezo mbalimbali. Miongoni mwa vigezo hivyo ni kigezo
cha upatanishi wa kisarufi au kigezo cha kisintaksia.
Upatanishi wa kisarufi ni hali ya viambishi vya
maneno ndani ya tungo kukubaliana na kushikamana ili kuleta maana
iliyokusudiwa. Upatanishi wa kisarufi unaweza kuonekana kati ya vipashio
mbalimbali vya tungo:
Mifano:
Unyasi
umeota. = Nyasi zimeota.
Kiazi kitamu.
= Viazi vitamu.
Huyu
mnene. = Hawa wanene.
Huyu
anakuja. = Hao wanakuja.
Mtu
ambaye. = Watu
ambao.
Mtu
aliyesafiri. = Watu waliosafiri.
Aina za tungo
Tungo
ni matokeo ya kupanga pamoja vipashio sahili ili kujenga kipashio kikubwa
zaidi.
Aina
za tungo ni:
Neno
Neno
ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa na kuandikwa na zinaleta maana.
Mfano, mama.
Kirai
Ni
tungo yenye neno moja au zaidi lakini haina muundo wa kiima na kiarifu. Mfano,
mtoto yule.
Kishazi
Kishazi
ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe
uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea
chenyewe. Mfano, mbuzi aliyepotea.
Sentensi
Sentensi
ni tungo yenye kiima na kiarifu na inaleta maana. Mfano, mama anapika pilau
jikoni.
Aina za Virai
Kuna
aina tano za Virai:
-
Virai nomino
-
Virai vitenzi
-
Virai vivumishi
- Virai
vielezi
-
Virai viunganishi
Virai nomino
Kirai
nomino ni kirai ambacho muundo wake umekitwa kwenye nomino.
Miundo ya Virai nomino
I. Nomino
peke yake. Mfano: chaki, dada, Juma.
II. Nomino
mbili au zaidi. Mfano: Baba na mama.
III. Nomino
na kivumishi kimoja au kadhaa. Mfano: Mtu mnene.
IV. Nomino
na sentensi. Mfano: mtoto aliyemletea mama yake kuni jana.
V. Nomino,
kivumishi na sentensi. Mfano: kijana yule mrefu aliyemnunulia mwanangu soda
jana asubuhi.
VI. Nomino
na Kirai kivumishi. Mfano: mzee mwenye duka kubwa kabisa kule kijijini.
Miundo ya virai vitenzi
I. Kitenzi
peke yake. Mfano, amekufa.
II. Kitenzi
na nomino moja. Mfano, amempiga Juma.
III. Kitenzi
na nomino mbili. Mfano, amempa mtoto chakula.
IV. Kitenzi
na kitenzi. Mfano, anapenda kusoma.
V. Kitenzi
na nomino na kitenzi. Mfano, anamfundisha mtoto kusoma.
Miundo ya virai vivumishi
I. Kivumishi
na kielezi chake. Mfano, zuri kabisa.
II. Kivumishi
na kirani nomino. Mfano, enye duka kubwa.
III. Kivumishi
na kirai kitenzi. Mfano, enye kupenda mambo makubwa.
IV. Kivumishi
na kirai kivumishi. Mfano, mwingine mwenye matatizo.
V. Kivumishi
na kirai kiunganishi. Mfano, zuri wa kutamanika.
Aina za vishazi
Kuna
aina mbili za vishazi:
1. Kishazi
huru
Hiki
ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kikuu.
Mfano
Anacheza
mpira.
2. Kishazi
tegemezi
Hiki
ni kishazi ambacho kinatawaliwa na kitenzi kisaidizi.
Mfano
Mwalimu
aliyefundisha darasani
Aina za vishazi tegemezi
Vishazi
tegemezi vivumishi
Hivi
ni vishazi ambavyo hufanya kazi ya vivumishi.
Mfano
Samaki
aliyepotea jana
Vishazi
tegemezi vielezi
Vishazi
hivi hufanya kazi ya vielezi katika tungo.
Mfano
Kijana
alilala aliposemwa
Muundo
wa sentensi
Sentensi
ina sehemu kuu mbili:
Kiima
Ni
sehemu katika sentensi inayojaza nafasi ya mtenda au mtendewa wa jambo
linaloelezwa.
Mfano
Baba
anacheza mpira
Kiarifu
Ni
sehemu katika sentensi inayojazwa na maneno yanayoarifu tendo lililofanywa,
linalofanywa na litakalofanywa.
Mfano
Juma ni
mkulima.
Dhima za Vishazi
1. Kufanya
kazi ya kivumishi katika tungo.
Mfano,
chakula kilichopikwa jana
2. Kufanya
kazi ya vielezi katika tungo.
Mfano,
mtoto alilia alipopigwa.
Uchanganuzi
wa sentensi
Uchanganuzi
wa sentensi ni kitendo cha kuigawa sentensi katika sehemu mbalimbali ambazo
huunda sentensi hiyo.
Hatua muhimu katika uchanganuzi wa sentensi
1. Taja
aina ya sentensi, kama ni sahili, ambatano au changamano.
2. Taja
sehemu zake kuu, yaani kiima na kiarifu.
3. Taja
sehemu kuu za kiima na kiarifu au za kirai nomino na kirai kitenzi.
4. Taja
aina zote za maneno zilizomo katika sentensi hiyo.
5. Iandike
upya sentensi hiyo.
Kuchanganua sentensi kwa njia ya majedwali
Mama
anapika chakula.
Sentensi
Sahili |
||
KN |
KT |
|
N |
T |
N |
Mama |
anapika |
Chakula. |
Simba aliyeunguruma, amerudishwa mbugani.
Sentensi
Changamano |
|||
KN |
KT |
||
N |
TS |
T |
E |
Simba |
aliyeunguruma |
amerudishwa |
Mbugani. |
Mama
anapika chakula na baba anafua nguo.
Sentensi Ambatano |
||||||
S1 |
|
S2 |
||||
KN |
KT |
|
KN |
KT |
||
N |
T |
N |
U |
N |
T |
N |
Mama
|
anapika |
chakula |
na |
baba |
anafua |
Nguo. |
Maswali Ya Kiswahili Kidato cha Tatu Mada ya Ngeli za Nomino
1. Upatanisho
wa kisarufi hufanya nomino mbalimbali kuwa katika kundi moja. Fikiria nomino
tano na kwa kutumia sentensi moja kwa kila nomino zipange katika makundi yake.
2. Uchanganuzi
wa sentensi hufanyika hatua kwa hatua. Ukitumia hatua hizo changanua sentensi ifuatayo
kwa njia ya jedwali Wale wawili watakuwa wamepimwa virusi vya UKIMWI hivyo afya
zao zitakuwa nzuri.
3. Eleza
tofauti za msingi mbili (2) zilizopo kati ya kirai na kishazi. Toa mifano
miwili kwa kila tofauti.
4. Ni
kigezo kipi kinachotumika katika kuunda ngeli za kimapokeo? Dhihirisha utumiaji
wa kigezo hicho kwa kutunga sentensi tano (5) za ngeli tofauti.
5. Eleza
maana ya upatanisho wa kisarufi. Fafanua jibu lako kwa kutoa mifano minne.
6. Kwa
kutumia mifano, taja miundo mitano ya kirai nomino.
7. “Upatanisho
wa kisarufi ni kigezo kimojawapo kati ya vigezo vya kuunda ngeli za nomino.” Thibitisha
dai hilo kwa kutunga sentensi ukitumia ngeli zifuatazo:
(a) UI
(b) LIYA
(c) UZI
(d) IZI
(e) UYA
8. Katika
kila sentensi uliyopewa, orodhesha vishazi huru katika Safu A na vishazi
tegemezi katika safu B.
(a) Ngoma hailii vizuri kwa kuwa imepasuka.
(b) Watoto walioandikishwa watakuja kesho.
(c) Kiongozi atakayefunga mkutano amepelekewa
taarifa.
(d) Mtawatambua walio wasikivu.
(e) Kitabu ulichopewa kina kurasa nyingi.
9. Fafanua
dhana zifuatazo kisha tunga sentensi moja kwa kila dhana:
a) Kirai
b) Kishazi
c) Sentensi
10. Tunga
tungo moja kwa kila kipengele (i) – (iv) ukizingatia viambajengo vya kila moja:
I. Kishazi tegemezi + Kishazi huru
II. Kishazi huru
III. Kishazi tegemezi
IV. Kishazi huru + Kishazi huru