Uhistoria Mpya Katika Diwani ya Chini ya Mwembe
Historia
huumba matini ya kisanaa tunayoyaona, kuyasikia na kuyasoma. Tumia nadharia ya
uhistoria mpya kusawiri uhusiano uliopo kati ya historia ya maendeleo ya taifa
la Tanzania na maudhui ya diwani ya Chini ya Mwembe (2017) ya Eric F. Ndumbaro
na Gloria D. Gonsalves.
Jibu
Nadharia
ya uhistoria mpya ni nadharia ambayo inaeleza uhusiano uliopo baina ya
historia na fasihi. Inatambulika kwamba wahakiki wa uhistoria mpya wa
Kimarekani ndio wanaotambulika kwa kuenea kwa mkabala wa uhistoria katika
fasihi katika miaka ya 1980 na ile ya 1990. Wahakiki wa uhistoria mpya wao
walisoma matini za kifasihi kama zao la kitu kinachotokana na mazingira ya
kipindi mahususi cha kihistoria. Miongoni mwa majina makubwa ya wahakiki wa
mkabala wa uhistoria mpya wa Marekani ni Stephen Greenblattt na Louis Montrose.
Wamitila
(2008), anajadili kipengele kingine muhimu kinachoshughulikiwa na wanauhistoria
mpya. Anadai kwamba kwa wanauhistoria mpya, matukio ya kihistoria siyo lazima
yaonekane yote kwa wazi kabisa. Kuna matukio mengine yanaweza kujitokeza kwa
njia ambayo si ya wazi sana, lakini bado tukaweza kubaini matukio halisi ya
kihistoria yanayojadiliwa.
Hivyo
basi kuna uhusiano wa karibu sana kati ya fasihi na historia, hususani riwaya.
Kukna mambo mengi yanayochangiwa kwa pamoja kati ya fasihi na historia. Mambo
hayo ni pamoja na ubunaji, mahali, wakati, usimulizi, matukio halisi ya
kihistoria na suala la ukadinaji katika kueleza utokeaji wa matukio au jambo
fulani.
Maudhui
ni jumla ya mawazo yote ya mwandishi katika kazi ya fasihi. Maudhui hujumuisha
vipengele vifuatavyo: dhamira, ujumbe, migogoro, falsafa na mtazamo.
Diwani
ya Chini ya Mwembe ni kusanyiko la mashairi tofauti yanayogusa maisha ya
mwanadamu. Mashairi yaliyopo yanatambua hisia mbalimbali kama mapenzi, furaha,
Amani na wasiwasi, uchungu na hasira. Maisha bila hisia ni kifo. Diwani hii
inahamasisha watu watafute mti wa mwembe utakaosaidia kutafakari hisia za
maisha.
Uhusiano
uliopo kati ya historia na maendeleo ya taifa la Tanzania na madhui ya diwani
ya Chini ya Mwembe yanajadiliwa:
Kwanza
tunaona mawazo ya kimvuvumko na mwamko mpya kuhusu historia. Mawazo haya
yanaonekana katika shairi la UJUZI WA FUNDI NGUO. Mshairi anakosoa tabia mbaya
ya fundi nguo. Anasema,
“Umaarufu
unao, ila punguza uongo,
Utakuja
adhirika, mbele ya kadamnasi,
Toa
miadi ya kweli, epuka msongamano,
Fundi
huyu fundi gani? Kila nguo anashona.”
Ubeti
huu unabeba malalamiko ya miaka mingi kuhusu mafundi. Mafundi wamekuwa si waaminifu
kiasi cha kuharibu kazi. Upo uhusiano kati ya historia hiyo ya mafundi na
maendeleo ya taifa. Fundi anaweza kufananishwa na kiongozi yeyote asiye
muadilifu ambaye ameshindwa kuleta maendeleo katika jamii yake.
Dhamira
inayopatikana katika shairi hili ni umuhimu wa kusema ukweli. Mshairi anamuonya
fundi,
“Fundi
acha longolongo, mara leo mara kesho,
Na
kesho ikishafika, kauli kubadilisha,
Nenda
urudi jioni, vimebaki vishikizo,
Sifa
zako zatambaa, na kupita vizingiti.”
Ni
vyema mafundi wakawa wakweli kwani wanayo nafasi ya kufanya mabadiliko na
kubadili historia.
Jambo
jingine ni kujirudia kwa historia. Katika shairi la SAFARI YA KANAANI, mshairi
anatamani kuona historia ikijirudia. Katika ubeti wa pili mshairi anasema,
“Upo
wapi ewe Joshua, Joshua wake Tanzania,
Ewe
Rabuka, twasikia twatii anayotwambia.”
Mshairi
anatamani historia ya wana wa Israel ijirudie ili kuleta ukombozi katika nchi
ya Tanzania. Anatamani kumuona Joshua akirudi tena.
Dhamira
inayopatikana katika shairi hili ni hamu ya mabadiliko. Wtu wamechoshwa na hali
ya sasa, wanatamani kuona mabadiliko yakipatikana ili kuweza kuleta maendeleo,
mshairi anasema,
“Ni
nchi yetu ya ahadi, tangia enzi za Farao,
Kanaani
hatuna budi, hilo ni letu kimbilio.”
Kauli
ya mshairi imebeba matarajio ya Watanzania wengi ambao wanatamani kuona
mabadiliko yakitokea. Watanzania wamechoka kuonewa na kufanyiwa mambo yote
yasiyofaa. Hivyo basi, shairi hili linabeba malalamiko ya miaka mingi. Tangu
enzi za ukoloni Watanzania wanatamani kuona mabadiliko na mpaka sasa
hawajayaona.
Pia,
mshairi anapinga maneno ya wahenga ili kusaidia kuleta maendeleo ya taifa.
Katika shairi la YA WAHENGA YAKAPIMWE. Mshairi anasema,
“Bado
nipo fikirani, wema hawana maisha!
Mantiki
yake nini? Wabaya wana maisha?
Ni
msemo wa zamani, wengi ulitupotosha.”
Mshairi
anapinga msemo usemao wema hawana maisha ambao umesemwa na wahenga miaka mingi
iliyopita. Mshairi anaona kuwa, kuendelea kukubaliana na msemo huu ni kuruhusu
maovu na ubaya. Vitu hivi vikizidi, maendeleo ya jamii hukosekana.
Ujumbe
unaopatikana katika shairi hili ni, siyo kila kilichosemwa na wahenga ni
sahihi, bali zipo kauli zao zenye utata na zisipotumiwa vizuri zinaweza
kuharibu. Mshairi anasema,
“Sio
yote walosema, yamejaa ufaafu,
Hili
napinga mapema, tena pasipo kashifu,
Fikirani
nimekwama, natema kwa utiifu.”
Hivyo
basi, katika jamii, watu wasiache kutenda wema kwa madai kuwa wema hawadumu.
Wema ni chanzo cha maendeleo na wema ndiyo msingi wa ubinadamu.
Vile
vile tunaona nafasi ya historia katika jamii. Katika shairi la AMANI mshairi
anasema,
“Amani
kuichezea,
Utakuja
ijuita,
Hakika
nakuambia,
Wengine
watamania.”
Mshairi
anaonesha umuhimu wa Amani ambayo Tanzania imeendelea kuwa nayo. Katika
historia, kwa miaka mingi Tanzania inajulikana kama kisiwa cha Amani. Hivyo,
chondechonde tusithubutu kuichezea Amani yetu.
Ujumbe
unaopatikana katika shairi hili ni, Amani ni kitu muhimu na kinapopotea, athari
kubwa hujitokeza. Mshairi anasema,
“Amani
kuipoteza,
Hakika
nawaapiza,
Tutaishi
kwenye kiza,
Kama
fuko mashimoni.”
Mshairi
anaonesha umuhimu wa historia yetu ya Amani ili kuleta maendeleo ya taifa la
Tanzania. Ni ukweli usiopingika kuwa, bila Amani hatuwezi kuwa na maendeleo.
Pia,
tunaona nafasi ya mwanadamu katika kuibadili historia yake. Katika shairi la
MWALIMU WA UBUNIFU, mshairi anampongeza mwalimu ambaye amembadilisha kutoka
asiyejua mpaka anayejua. Mshairi anasema,
“Mwalimu
wa ubunifu, fanaka nakuombea,
Kamwe
sitaki kufuru, mazuri kukyachimbia,
Nitasema
kwa uhuru, mambo ulonitendea,
Mwalimu
wangu hodari, kunifanya mbunifu.”
Ni
dhahiri kuwa, mshairi hakuwa mbunifu ila amepata ubunifu huo kutoka kwa mwalimu
wa ubunifu.
Mshairi
ana mtazamo wa kimapinduzi. Anaamini kuwa, mwanadamu ni chanzo cha mabadiliko
kama alivyo mwalimu wa ubunifu. Anasema,
“Bidii
kipaji chake, uzembe ugonjwa wake,
Uvivu
ni mwiko kwake, kujituma hobi yake,
Uchoyo
ni sumu yake, hupenda aeleweke,
Mwalimu
hongera sana, vipaji umeibua.”
Mshairi
anabainisha kuwa, bidi na kujituma ndiyo vyanzo vya maendeleo. Mshairia
anawapongeza walimu ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuelimisha.
Hoja
nyingine ni historiografia ya kitaifa au ya kimapinduzi. Katika shairi la
WAMENIACHIA UHAI, mshairi analaani vikali ukoloni mamboleo ambao umefunga furs
azote na kutuachia uhai pekee. Mshairi anasema,
“Wamenifunga
miguu, ningekuja kukuona,
Siwezi
kukujongea.
Wameniziba
mdomo, ningesema ukweli,
Nashindwa
nawe kuongea.
Wamenifunga
mikono, ningekushika mkono,
Siwezi
kushikilia.
Wamenifunga
machoni, kweli ningekutazama,
Siwezi
kuangalia.
Lakini
nawashukuru, uhai wameniachia,
Kwani
bado napumua.
Japo
hewa si safi, lakini nawashukuru,
Hawajaniziba
pua.”
Ni
kweli kwamba mataifa ya Afrika hayana uhuru wa kufanya lolote isipikuwa kutii
amri za mabeberu.
Ujumbe
unaopatikana katika shairi hili ni mataifa ya Afrika yaungane pamoja kupambana
na ukoloni mamboleo. Ukoloni mamboleo unaweza kuondolewa kwa kuwa na viongozi
wazuri, teknolojia na uchumi wa kujitegemea.
Kwa
kuhitimisha, historia huumba matini ya kisanaa. Nadharia ya uhistoria mpya
imesawiri uhusiano uliopo kati ya historia na maendeleo ya taifa la Tanzania
ikiwa ni pamoja na kutaja vipengele vya maudhui kama: dhamira, ujumbe na
msimamo. Hivyo basi, historia inayo nafasi yake katika kazi za fasihi na hakuna
sababu ya kuipuuza.
Marejeo
Mushengyezi,
A. (2003). Twentieth Century Literary
Theory. Kampala: MukonoPublishing Company Ltd.
Ndumbaro,
E na Gonsalves G. (2017) Chini ya Mwembe.
Njogu,
K na R. Chimera (1999). Ufundishaji wa
Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: The Jommo Kenyatta Foundation.
Senkoro,
F.E.M.K. (1987). Fasihi na Jamii. Dar
es Salaam: Press and Publicity Centre.
Unahitaji Kufanyiwa Swali Lako? Gusa Hapa Kuwasiliana Nami.