Dhima za Kategoria za Virai katika Lugha Kisintaksia
Lugha ya Kiswahili inazo tungo nyingi na miongoni mwa tungo hizo ni tungo kirai. Tungo zingine ni tungo neno, kishazi na sentensi. Kategoria za virai ni sifa bainifu zinazoambikwa kwenye aina za virai. Kwa upande wa maana, tungo kirai ni kipashio kidogo cha kimuundo chenye neno moja au zaidi ambacho hakina muundo wa kiima (K) na kiarifu (A). Kirai huwa na neno kuu moja linalotawala. Neno hilo linalotawala ndilo huwa aina ya kirai. Kategoria ya virai inajumuisha kirai nomino, kirai kivumishi, kirai kitenzi, kirai kielezi na kirai kihusishi. Zifuataza ni dhima za kategoria za virai katika lugha ya Kiswahili Kisintaksia.
Kirai nomino kina dhima ya kuwa kiima, yambwa, yambiwa, kijalizo cha kirai kihusishi
na kinaweza kukaa mahali pengine popote ambapo nomino inakaa. Kwa mfano: Askari
waaminifu waliwakamata wahalifu wetu wote kwa siku moja. Askari imetumika kama
kiima cha sentesi hiyo. Katika kirai nomino, neno kuu ni nomino.
Kirai
kitenzi kina dhima ya kuwa kiarifu. Kwa mfano, mama anapika chakula cha baba
yake na baba. Katika mfano huo wa sentensi neno Anapika ni kiarifu na neno mama
ni kiima. Hivyo kirai kitenzi kimetimiza dhima yake ya kuwa kiarifu ama kirai
kitenzi kimefanya kazi ya kuwa kiarifu. Kirai kitenzi ni kirai ambacho muundo
wake hutawaliwa na kitenzi.
Kirai
kivumishi kina dhima ya kuwa kikumushi cha kirai nomino. Kwa mfano, Kijana
mzuri mshamba. Katika mfano huo, mzuri mshamba imetumika kukumusha nomino
kijana. Pia, kirai kivumishi kina dhima ya kuwa kiima katika sentensi. Kwa
mfano, wakubwa wale. Kirai kivumishi ni kirai ambacho neno lake kuu ni
kivumishi.
Kirai
kielezi kina dhima ya kuwa kikumushi cha kirai kitenzi. Kwa mfano, anaruka
kichurachura. Katika mfano huo, neno kichurachura ni kikumushi cha kitenzi
anaruka. Pia kina dhima ya kuwa kiima cha sentensi kwa mfano chumbani kwangu.
Katika mfano huo, neno chumbani kwangu limetumika kama kiima. Kirai kielezi ni
kirai ambacho neno lake kuu ni kirai.
Kirai
kihusishi kina dhima ya kuwa kikumushi cha nomino kwa mfano, matawi ya miti.
Pia, kikumushi cha kitenzi (Mwalimu amesimama kwa hofu kubwa). Pia, kirai
kihusishi kinafanya kazi kama kiwakilishi. Kwa mfano, kwa mganga kumewekwa dawa
nyingi. Kirai kihusishi ni aina ya kirai ambacho neno lake kuu ni kihisishi.
Hivyo
basi, kategoria ya virai katika lugha ya Kiswahili ina dhima zake kama
ilivyoelezwa hapo juu. Virai hufanya kazi kubwa ambayo imesaidia kuipa lugha
maana. Uanishaji wa virai umejikita katika aina za maneno, yaani, aina za virai
zinatokana na aina za maneno. Kwa kutumia kigezo hicho ndiyo tumepata kategoria
hizo za virai zilizojadiliwa.