Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta | Sehemu ya Tano
Baada ya siku tatu bila kupita mitaa yake Asi huko
Mwananyamala ndanindani, nilipita tena ili niweze kumuona msichana huyu. Hali
ilikua tofauti kuliko siku zote, msichana hakuwepo. Nilitazama kama kweli ni
nyumba ileile ambayo tangu nianze kupita sijawahi kumkosa akiwa kakaa
kibarazani, ilikuwa nyumba ileile na msichana hakuwepo. Hata hivyo sikuwa na
wasiwasi, nilihisi huenda alikuwa na kazi humo ndani.
Nilipita tena siku iliyofuata, msichana hakuwepo.
Nikapita siku nyingine, hakuwepo, nikapita tena na tena mpaka chovya chovya
ikamaliza buyu la asali, lakini msichana hakuwepo. Hapo nikapatwa na hofu, hofu
ya kupotea kwa mwanamke aliyekula pesa zangu. Shilingi halali za Kitanzania
elfu kumi na tisa. Pengine hazikuwa zile pesa, kwani ni pesa kidogo sana
zisizotosha hata kununua simu ndogo ya Kichina, pengine nilianza kumpenda Asi,
binti mdogo aliyekuwa na tabasamu pana, mwepesi kuzoea watu tena aliyechangamka
vyema. Basi baada ya pitapita ya siku nyingi bila kumuona, nikaahidi kumtafuta
mpaka nimpate.
Soma: Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta |Sehemu ya Sita