Jinsi ya Kuomba Chuo kwa Usahihi
Kama umehitimu kidato cha
sita au umehitimu chuo kwa ngazi ya stashahada (diploma) na una sifa za kuomba
chuo, maelekezo haya yatakusaidia uombapo chuo.
Kwanza tufahamu ni mtu gani mwenye sifa za kuomba chuo?
Kwa mujibu wa mwongozo wa TCU kuhusu sifa za kuomba chuo, wamegawanya waombaji katika makundi kadhaa.
Miongoni mwa makundi hayo ni wale wanaoomba kutoka kidato cha sita, na waombaji
wanaotoka vyuo vya kati.
Sifa za mwombaji Kutoka kidato cha sita
Aliyemaliza kidato cha sita
kabla ya mwaka 2014 anatakiwa awe na ‘principle passes mbili zinazoleta jumla
ya alama 4.
Mgawanyo wa alama umekaa
katika mfumo huu: (A=5; B=4; C=3; D=2; E=1; S=0.5)
Aliyemaliza kidato cha sita
mwaka 2014 na 2015 anatakiwa awe na ‘principle passes’ mbili (C na kuendelea)
akiwa na jumla ya alama 4 katika masomo mawili.
Mgawanyo wa alama umekaa
katika mfumo huu: (A=5; B+=4 B=3; C=2; D=1; E=0.5)
Aliyemaliza kidato cha sita
mwaka 2016 na kuendelea anatakiwa awe na ‘Principle passes’ mbili yenye jumla
ya alama 4 katika masomo mawili.
Mgawanyo wa alama umekaa
katika mfumo huu: (A=5; B=4; C=3; D=2; E=1; S=0.5)
Mwanafunzi mwenye C na E anaweza kupata chuo?
Ndiyo, anaweza kupata chuo.
Kwa sababu C ina alama tatu na E ina alama moja, hivyo anakuwa amefikisha jumla
ya alama nne zinazotakiwa.
Sifa hizo, zinaelezwa katika jedwali hili:
Kwa wanafunzi wanaoomba kozi
za afya, wanatakiwa angalau wawe na D tatu katika masomo yao na wawe na jumla
ya alama 6.
Sifa za Kuomba Chuo kwa Wenye Diploma
Awe amefaulu masomo manne
kutoka kidato cha nne. Masomo hayo, yasiwe ya dini. Kufaulu maana yake awe
amepata angalau alama D.
Pia, awe amepata wastani wa
GPA ya 3.0 katika matokeo yake ya diploma.
Sifa hizo kwa ujumla,
zinaonyeshwa katika jedwali hili:
Kwa mwanafunzi mwenye sifa, anatakiwa kuomba chuo kupitia
njia ya mtandao. Maombi yanaombwa moja kwa moja katika chuo husika na kwa kila
ombi utakalofanya, gharama yake ni tsh. 10,000/=.
Inashauriwa mwanafunzi aombe angalau vyuo vitatu, endapo
ataomba vyuo vingi zaidi, basi visizidi vitano. Kwa mfano, kwa mwanafunzi
anayetaka kusomea fani ya Ualimu, anaweza kuomba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
DUCE na Mkwawa.
Baada ya maombi yako ya kwanza, endelea kufuatilia majibu
ya dirisha la kwanza. Katika dirisha la kwanza, unaweza kupata chuo ulichotaka
au unaweza kukosa kwa sababu ya ushindani. Usiwe na wasiwasi, dirisha la pili
litafunguliwa na utaelekezwa vyuo vyenye nafasi ambazo unaweza kutuma maombi
yako.
Hivyo basi, wanafunzi wanashauriwa kabla ya kuomba vyuo,
wasome mwongozo kutoka ‘TCU guide book’ ili wafanye maombi sahihi na wasipoteze
pesa zao kwa kufanya maombi ambayo hayaendani na sifa zao.
Soma: Jinsi ya Kuomba Mkopo
Kwa wanafunzi wanaohitaji usaidizi wa kuombewa vyuo,
tunatoa huduma hiyo kwa punguzo la bei. kwa wale wanaoomba vyuo vitatu, gharama
yetu ni tsh. 50,000/= tu, mgawanyo wa malipo ni, 30,000/= itatumika kama malipo
kwa vyuo husika, na tsh. 20,000/= itatumika kama gharama ya kufanyiwa maombi,
Gusa Hapa kuwasiliana na Mwalimu na kuanza kufanyiwa maombi yako.