Jinsi ya Kuomba Mkopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu
Bodi ya mikopo ya elimu ya
juu (HESLB) hujihusisha na utoaji mikopo kwa wanafunzi wanaotaka kusoma elmu ya
juu lakini pengine hawana uwezo wa kumudu gharama hizo hivyo kuhitaji
kukopeshwa. Taasisi hii ilianza kufanya kazi mnamo mwaka 2005.
Kwa mujibu wa chapisho la
bodi ya mikopo, haya ni maelekezo ya kuzingatia kwa waombaji wote:
Mambo ya kuzingatia kwa waombaji mkopo
Kabla ya kuomba mkopo, hakikisha umesoma maelekezo ya kuomba mkopo.
Namba ya kidato cha nne
inayotumika kuomba mkopo, iendane na namba ya kidato cha nne iliyotumika kuomba
chuo.
Wanafunzi waliorudia
mitihani yao, waorodheshe namba zao zote za mitihani.
Hakikisha kwamba, nyaraka zote
unazoambatanisha katika maombi ya mkopo, ziwe zimethibitishwa (verified) na
mamlaka husika zinazotambulika.
Hakikisha kwamba, cheti cha
kuzaliwa na kifo vithibitishwe na RITA, kwa upande wa Zanzibar, vithibitishwe
na ZCSRA.
Vyeti vya kuzaliwa vya wanafunzi
waliozaliwa nje ya nchi na vyeti vya vifo kwa wazazi wa Tanzania waliofariki
nje ya nchi, vithibitishwe katika barozi za nchi hizo zinazopatikana nchini
Tanzania.
Hakikisha kwamba, fomu yako
ya maombi imejazwa kwa ukamilifu na imesainiwa kabla ya kutumwa.
Hifadhi nakala baada ya
kutuma maombi.
Waombaji wafahamu tarehe ya
mwisho ya kutuma maombi.
Tunasisitiza tena kwa mara
nyingine kuwa, kabla ya kuomba mkopo, mwanafunzi asome maelekezo yote, japo ni
marefu, jitahidi usome yote kwa ukamilifu.
Soma: Jinsi ya Kuomba Chuo
Kwa wanafunzi wanaohitaji usaidizi wa kuombewa mkopo, tunatoa huduma hiyo kwa punguzo la bei. Gharama yetu ni Tsh. 50,000/= tu, mgawanyo wa malipo ni, Tsh. 30,000/= itatumika kama malipo kwa bodi ya mikopo, na Tsh. 20,000/= itatumika kama gharama ya kufanyiwa maombi, Gusa Hapa kuwasiliana na Mwalimu na kuanza kufanyiwa maombi yako.