Mtihani wa Kiswahili 1 Kidato cha Sita 2024 1

Mtu aliyevaa mavazi meusi kasimama nje ya jumba kubwa jeupe

Muda: Saa 3

Maelekezo

1. karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali nane.

2. Jibu maswali yote katika sehemu A na maswali matatu kutoka sehemu B. swali la tano ni la lazima.

3. Sehemu A in alama arobaini na sehemu B ina alama sitini.

4. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.

5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.

6. Andika namba yako ya mtihani au jina katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

Sehemu A (Alama 40)

Jibu maswali yote.

1. Soma kifungu cha habari kisha jibu maswali yanayofuata:

Utawala bora ni hali ya viongozi kusimamia vyema maslahi ya taifa lao. Ni kitendo cha kutenda haki kwa wote na kuhakikisha maisha mazuri kwa kila mmoja.

Kiongozi anaposhindwa kutawala vyema, wananchi hupatwa na kihoro hasa pale ndugu zao wanapoanza kuuawa kwa sababu ya kukosoa serikali. Serikali inayoua watu wake haifai hata kidogo.

Ni vyema kama viongozi watasimamia demokrasia kwani demokrasia ni utawala wa watu wote tena unaojali maslahi ya kila mwananchi. Kinyume na hapo mambo hayawezi kwenda.

Katika nchi isiyofuata demokrasia, ni kawaida kuona wananchi wakitaharuki kwa kila jambo. Mara leo wamebomolewa nyumba zao, kesho wamepigwa na askari na kesho kutwa wamedhulumiwa mashamba.

Ili wananchi waondokane na vinyongo vyao, tunarejea palepale, utawala bora unahitajika. Utawala ambao kiongozi huongoza kwa kuzingatia sifa zote za kiongozi bora.

Maswali

a. Andika kichwa cha habari chenye maneno yasiyozidi matatu.

b. Orodhesha mawazo makuu matatu yanayopatikana katika aya ya pili.

c. Taja faida moja ya serikali kusimamia utawala bora.

d. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu cha habari.

i. Demokrasia ii. Taharuki iii. Kihoro iv. Kinyongo

2. Taja mambo muhimu matano yanayoweza kumsaidia mtumiaji wa lugha kuwa mahiri.

3. Fafanua kwa mifano dhana zifuatazo:

i. Utata katika lugha

ii. Rejesta

iii. Misimu

iv. Umahiri wa lugha

4. Bainisha dhima za mofimu zilizopigiwa mstari katika maneno haya:

i. Mkimbizi

ii. Hunun’gunika

iii. Asiyeridhika

iv. Watembeao

v. Amenialika

vi. Nimekufikia

vii. Tumejitakia

viii. Watamfurahisha

ix. Pangua.

Sehemu B (Alama 60)

Jibu maswali matatu, swali la nane ni la lazima.

5. Andika barua ya kiofisi yenye lengo la kukiri kupokea bidhaa ulizoagiza kutoka kampuni ya Mchumi Traders wa S.L.P 750 Mwanza. Bidhaa hizo ni jozi 50 za viatu vya ngozi, jozi 100 za soksi nyeupe, dazeni 100 za pensel, katoni 100 za sabuni ya mbuni na seti 150 za vikombe vya plastiki. Jina lako liwe Malingumu Sulubu wa S.L.P 1000 Magu.

6. Tathmini mchango wa serikali katika kukuza Kiswahili nchini Tanzania baada ya uhuru. Hoja sita.

7. Tathmini dai kuwa asili ya Kiswahili ni kiarabu kwa kutumia hoja tatu kisha onesha udhaifu wa dai hilo kwa kutoa hoja tatu.

8. Jibu maswali haya:

a. Onesha tofauti tano kati ya tafsiri ya kimawasiliano na tafsiri ya kisemantiki.

b. Tafsiri sentensi hizi kwenda lugha ya Kiingereza kwa kuzingatia tafsiri ya kisemantiki:

i. Zawadi anacheza netiboli/mpira wa pete

ii. Mama huenda sokoni kila jumamosi/kila jumamosi mama huenda sokoni.

iii. Anajua chanzo cha maradhi yake/ugonjwa wake.

iv. Shangazi yangu/mama mdogo wangu atapika chapati tamu.

v. Ninapenda kusoma riwaya za Kiswahili

vi. Walimu wanafanya kazi nzuri sana.

vii. Mkutano wa wiki tatu utakwisha leo.

viii. Kama watashinda watapewa zawadi.

ix. Ulisikia lakini hukutaka kuitika.

x. Usiende, labda kama una sababu ya msingi.

Pata Majibu Yote ya Mtihani Huu, Wasiliana Nasi Hapa

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2025

Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 1