Uandishi wa CV au Wasifu | Maswali na Majibu
Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi.
Nimekuwa nikiulizwa maswali mengi na watu mbalimbali kuhusiana na CV au Wasifu. Hapa nimeweka maswali ninayoulizwa sana pamoja na majibu yake.
1. CV au Wasifu ni nini?
CV au wasifu ni maelezo kuhusu mtu fulani ambapo maelezo hayo huangazia historia ya elimu pamoja na uzoefu wa kazi. Waajiri huhitaji CV yako ili iwarahisishie kukufahamu na kupata mawasiliano yako.
2. CV bora ina kurasa ngapi?
CV bora ina kurasa mbili hadi tatu. CV ya ukurasa mmoja haifai na CV yenye zaidi ya kurasa tatu haina vigezo.
Jifunze: Jinsi ya Kuandika Barua ya maombi ya Kazi
3. Wadhamini katika CV ni watu gani?
Wadhamini katika CV ni mtu yeyote anayekufahamu ambaye endapo atapigiwa simu na waajiri ataweza utoa maelezo kukuhusu. Mdhamini anaweza kuwa rafiki yako uliyesoma naye na sasa anafanya kazi fulani. Anaweza kuwa mwalimu aliyekufundisha au mwajiri wako wa zamani. Pia, mdhamini anaweza akawa mtu yeyote anayekufahamu bila kujali kazi yake. Anaweza kuwa mjasiriamali, mkulima na kazi yoyote.
4. Niweke wadhamini wangapi katika CV?
Waajiri wengi hutaka kati ya wadhamini wawili mpaka watatu. Hivyo weka wadhamini watatu.
5. Kama nimefanya kazi sehemu nyingi, niziandike zote?
Hapana. Usiandike sehemu zote ambazo umefanya kazi endapo ni nyingi. Kuandika sehemu zote kutafanya CV yako izidi idadi ya kurasa tatu zinazotakiwa. Endapo umefanya kazi sehemu nyingi, chagua sehemu tatu ambazo unaona zinaendana na kazi unayoomba, ziweke hizo katika CV yako.
6. Niweke maarifa gani katika CV yangu?
Weka maarifa yoyote uliyonayo. Kama unaweza kuendesha gari weka maarifa hayo. Kama unafahamu kutumia kompyuta andika. Unaweza kuweka maarifa ya jumla kama, kufundisha, kutafuta wateja, kusuluhisha migogoro na maarifa mengineyo.
7. Niandike CV yangu katika lugha gani?
Andika CV yako katika lugha yoyote. Inaweza kuwa Kiswahili au Kiingereza. Muhimu ni kwamba, kama tangazo la kazi limeandikwa kwa lugha ya Kiswahili, hakikisha CV utakayotuma iwe katika lugha ya Kiswahili. Endapo tangazo la kazi lipo katika lugha ya Kiingereza, CV yako iwe katika lugha ya Kiingereza. Kwa mtu ambaye bado anatafuta kazi, ni vyema akawa na CV zote mbili. Aliyoandika kwa kiswahili na ile iliyoandikwa kwa kiingereza. Muhimu ni kwamba: kazi nyingi za serikalini huandikwa kwa lugha ya Kiswahili na kazi nyingi binafsi, huandikw kwa lugha ya Kiingereza.
8. Waajiri husoma CV?
Ndiyo, waajiri husoma CV. Zipo kampuni ambazo haziishii kusoma CV yako pekee, bali huingia mpaka katika mitandao yako ya kijamii na kutazama unayoyafanya huko. Kampuni nyingi zinapotaka kuajiri, huwa zinatafuta mtu sahihi wa kuendana na kampuni hiyo, hivyo unapoandaa CV yako tambua kwamba itasomwa.
9. Ni upi mfano wa CV bora inayokubalika?
CV bora inayokubalika ni ile ambayo imeandikwa kwa kuzingatia kanuni bora za uandishi. CV bora haina mbwembwe nyingi kama rangi na mengineyo yasiyo muhimu. CV bora ni ile ambayo huandikwa kwa mwandiko mmoja tu, na rangi zinazoonekana ni nyeusi na nyeupe. Chini nimekuwekea mfano wa CV bora inayokubalika.
Interests: Reading Books, Running, and Teaching.