Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi ya Mauzo|Kiswahili

Barua za maombi ya kazi zikiwa zimepangwa.

Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi.

Huu ni mfano wa barua ya mtu anayeomba kazi ya mauzo katika kiwanda fulani. Mwombaji kazi huyu ana elimu ya shahada na anajieleza vyema.

Katika barua yake, amendika vyema anuani yake. Kwa kuwa hana sanduku la posta, ameanza na namba ya simu ikifuatiwa na barua pepe.

Katika kiini ametumia aya nne:

Aya ya kwanza ameeleza jinsi yake, umri pamoja na kazi anayoomba. Ameeleza alipoona tangazo la kazi, lakini hajaeleza ni tarehe gani tangazo hilo liliwekwa. Pengine hakuwa na uhakika ndiyo sababu ya kuacha kipengele hicho.

Aya ya pili anaeleza elimu yake. Katika kipengele hiki hatuoni uzoefu wa kazi. Tunarejea katika hoja kuwa, pengine mwombaji kazi huyu hakuwa na uzoefu wowote wa kuweka.

Aya ya tatu anaeleza kwa nini apewe kazi hii yeye na si mtu mwingine. Anafafanua kutokana na uzoefu wake, lakini uzoefu huu hakutuwekea katika aya ya pili. Pengine uzoefu wake haukuwa katika sekta rasmi, yeye anafahamu zaidi.

Aya ya nne anamaliza kwa kusema yupo tayari kwa usaili na anamatarajio chanya.

Namna ya uandishi iliyotumika, inawafaa watafuta kazi wote katika kitengo cha mauzo.

Simu: 0721 601 374,
Barua Pepe: slm@gmail.com,

DAR ES SALAAM.
14/08/2024.

Manager,

Julius Msote,

NIDA textile mills,

P.O.Box 25,
Mnazi Mmoja. 

Ndugu,

 

Yah: OMBI LA KAZI YA MAUZO (Storekeeper/sales)

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 27. Ninaomba kazi ya mauzo katika kiwanda chako kama ilivyotangazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Nina Shahada ya Ugavi na Manunuzi niliyotunukiwa na Chuo cha Usafirishaji cha Taifa mwaka 2024.

Kutokana na uzoefu wangu, elimu, uwezo wa kufanya kazi nilionao pamoja na kuwa na sifa zinazotakiwa, ninaamini kuwa ninastahili kupata kazi hii. Endapo nitapata kazi ninayoomba, nitafanya kazi kwa bidii na kutimiza majukumu yangu yote.

Nipo tayari kwa usaili siku yoyote nitakayohitajika. Vilevile, ninatarajia majibu mazuri kutoka kwako na nimeambatanisha nakala ya vyeti vyangu kwa uthibitisho zaidi. 

Wako mtiifu,

___________

AYATOLA AHMED ALLY

Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Fasihi ni Zao la Jamii | Harusi ya Dogoli na Vuta n’kuvute

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024