Mtihani wa Kiswahili 1 Kidato cha Sita 2024 NECTA

Ndege akiwa katulia katika tawi dogo la mti.
Muda: Saa 3

Sehemu A (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. soma shairi lifuatalo kwa makini kisha jibu maswali yanayofuata:

Majira pia Nipashe, taarifa nazitoa
Na redio niwabishe, kama ikiwafikia
Majirani niwapashe, jambo nilokusudia
Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni.

Ndege nawaelezea, tabia yake murua
kucheka yake tabia, kununa hakuzoea
Wageni wakiingia, fadhila huwatendea
Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni.

Tabia za firauni, hana ninawaapia
Na kuranda mitaani, si yake hiyo tabia
Marafiki wa Kihuni, hapendi kuwasikia
Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni.

Kisa niwaelezeni, tunduni nikamtoa
Msusa nambari wani, kisa si kisa alia
Hilo kosa namba wani, huzuni imenitia
Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni.

Lingine lilochangia, tunduni nikamtoa
Kosa sugu nadhania, sijui kama sawia
Kufuga ndege Songea, sijui kama sawia
Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni.

Mara aliposikia, mwingine nimechukua
Tundu akalibomoa, porini akakimbia
Goti nikampigia, katu kanikatalia
Ndege nimemfungua wafugaji chukueni.

Maswali

A. Andika kichwa kinachofaa kwa shairi ulilosoma kwa maneno yasiyozidi matano.

NDEGE NIMEMFUNGUA.

B. Mshairi anapotaja ndege katika shairi hili anamaanisha nini?

Ana maanisha mwanamke.

C. Taja tabia tatu za ndege anayezungumziwa katika shairi.

- Tabia ya kucheka na kununa hakuzoea.

- Tabia ya kutulia ndani. Hapendi kuranda mitaani.

- Kulialia bila sababu.

D. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi ulilosoma.

I. Murua

Kitu kizuri.

II. Firauni

Mtu mwenye tabia mbaya.

III. Kisirani

Mtu anayekasirika bila sababu.

E. Sababu ipi ilimfanya mshairi amfungulie ndege aliyekuwa akimpenda?

Mshairi alimfungulia ndege aliyekuwa akimpenda kwa sababu alikuwa analialia bila sababu.

F. Katika ubeti wa mwisho mwandishi anaeleza ndege alichukizwa na nini?

Ndege alichukizwa na kitendo cha kuchukua ndege mwingine.

G. Funzo gani unalipata kutokana na shairi ulilosoma?

Kuacha kisirani au tabia ya kulialia hovyo bila sababu yoyote ya msingi.

2. Onesha miundo mitano ya kiima na mitano ya kiarifu kwa kutoa mfano kwa kila moja.

Miundo wa kiima:

Nomino peke yake, mfano, baba

Nomino, kiunganishi na nomino, mfano, baba na mama

Nomino na kivumishi, mfano, baba yule

Kivumishi na nomino, mfano, yule baba

Kiwakilishi peke yake, mfano, mimi

Miundo ya kiarifu:

Kitenzi kikuu peke yake, mfano, amekuja

Kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu, mfano, aliyekula kaja

Kitenzi kishirikishi na kijalizo mfano, ni mkubwa

Shamirisho

Chagizo

3. Bainisha vishazi katika sentensi zifuatazo, kisha taja aina ya Kishazi ulichokibainisha:

A. Mwanafunzi aliyefaulu vizuri amepata ufadhili.

Mwanafunzi aliyefaulu-kishazi kisaidizi

Mwanafunzi amepata ufadhili-kishazi huru

B. Sikukuu ya sabasaba inakaribia mimi nitakwenda uwanjani.

Kishazi huru; nitakwenda uwanjani.

C. Mwanao akililia wembe mpe.

Kishazi tegemezi: mwanao akililia wembe mpe.

D. Ungemuona simba ungejificha mapema.

Kishazi tegemezi: ungemuona simba

E. Kisima ambacho kimejaa tope tupu wanachi hawakipendi.

Kishazi tegemezi: kisima ambacho kimajaa tope

Kishazi huru: Kisima wanachi hawakipendi.

4. Mtumiaji wa lugha ya Kiswahili anapaswa kuzingatia misingi gani? Fafanua kwa misingi mitano kwa kutumia mfano kwa kila moja.

Mazingira

Mazingira humwamulia mtu namna ya kutumia lugha. Kwa mfano, lugha ya hotelini ni tofauti na lugha ya kanisani. Kutokana na mazingira, tunaweza kupata lugha ya: hotelini, shuleni, ofisini, kanisani na mitaani.

Uhusiano baina ya wahusika

Uhusiano baina ya wahusika, hufanya matumizi ya lugha yabadilike. Mfano, lugha ya marafiki vijana, imejaa misimu mingi na maneno yasiyo na adabu. Lugha ya baba na mtoto ina maneno yenye heshima. Pia, uhusiano baina ya wahusika unatupatia lugha ya mtu na mpenzi wake, mwalimu na mwanafunzi wake, meneja na wafanyakazi wa chini yake n.k

Mada ya mazungumzo

Mada ya mazungumzo ndiyo inayokuamulia maneno ya kusema. Kutokana na mada ya mazungumzo tunapata lugha ya: kibiashara, kitaaluma, mahubiri, kisiasa, kisheria n.k

Madhumuni ya mazungumzo

Watu wanapotumia lugha huwa na lengo. Kutokana na malengo hayo, lugha inayotumiwa nayo hubadilika ili kuendana na lengo la mzungumzaji. Kama lengo la mzungumzaji ni kuomba msaada fulani, atatakiwa kutumia lugha ya unyenyekevu kama, ‘tafadhali,’ ‘samahani,’ n.k kama lengo ni kutoa amri, lugha ya mzungumzaji itakuwa na maneno yenye kuashiria amri kama vile, ondoka, cheza, soma, imba n.k

Utanzu wa mawasiliano

Utanzu wa mawasiliano unanafasi kubwa katika uteuzi wa lugha. Kama ni utanzu wa hotuba, majadiliano, masimulizi n.k matumizi ya lugha lazima yaendane na utanzu huo.

Pata Majibu ya Maswali yaliyobaki kwa Tsh. 1,000/= tu, Wasiliana na Mwalimu Hapa

Sehemu B (Alama 60)

Jibu maswali matatu kutoka sehemu hii. Swali la tano ni la lazima.

5. Fafanua sifa sita za tafsiri ya matini za kisayansi na kiteknolojia kwa kutoa mfano kwa kila moja.

6. Andika insha ya maneno yasiyozidi mia nne na yasiyopungua mia tatu na hamsini kuhusu sababu na athari za ndoa za utotoni.

7. Vyombo vya habari vilikuwa na mchango gani katika kukuza Kiswahili nchini Tanganyika wakati wa ukoloni? Fafanua kwa kutumia hoja tano.

8. Kamati ya lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki iliyoanzishwa mwaka 1930 kwa lengo la kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ilikuwa na majukumu mbalimbali. Eleza majukumu sita yaliyotekelezwa na Kamati hiyo.

Pata Majibu ya Maswali yaliyobaki kwa Tsh. 1,000/= tu, Wasiliana na Mwalimu Hapa

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Notes za Kiswahili Kidato cha Pili | Form Two

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2025