Mtihani wa Kiswahili 2 Kidato cha Sita 2024 NECTA Majibu

Mvua inanyesha katika eneo lenye kimbweta na miti mirefu.

Muda: Saa 3

Sehemu A (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Wasanii huongozwa na mbinu mbalimbali katika kutunga kazi za fasihi simulizi. Onesha mbinu zinazotumiwa na wasanii katika kutunga igizo kisha tunga igizo fupi linalohusu madhara ya ukeketaji.

Taratibu za kutunga maigizo

- Kuchagua tukio la kuigizwa

Tukio hilo, liwe na mchango chanya katika jamii, ikiwemo kuelimisha.

- Kuchagua mahali pa kutendeka kwa jambo

Mahali panaweza kuwa: ofisini, shuleni, kijijini barabarani n.k

- Kuamua mtindo wa kuwasilisha jambo la kuigizwa

Hapa mwandishi anaweza kutumia fumbo, vichekesho n.k

- Kupanga hoja kuu zinazojenga maudhui ya igizo

Maudhui hujikita katika migogoro au mivutano. Masuluhisho ya migogoro yanatakiwa kupatikana. Mfano, jambazi kuu hukamatwa mwisho wa igizo.

- Kuweka mpangilio wa maonyesho

Mtunzi atumie mpangilio mzuri ambao utasaidia wasomaji waweze kuelewa kazi yake.

- Kubuni wahusika

Mwandishi anashauriwa kubuni wahusika wenye sifa tofauti: wanene, weupe, weusi, warefu, wafupi n.k pia, wahusika hawa wawe na uhalisia na wahusika halisi waliopo katika jamii.

Mwanafunzi atunge igizo linalohusu madharaya ukeketaji kwa kuzingatia mfano wa igizo hili:

Mfano wa igizo

Bodaboda na Binti

Bodaboda: Habari yako dada. (Akisimamisha pikipiki yake.)

Msichana: Nzuri, shikamoo!

Bodaboda: Aaaah, usinizeeshe binti, vipi, panda nikupeleke, mtoto mzuri kama malaika, haifai kutembea kwa mguu.

Msichana: Sitaki, niache nisome, ukiendelea kunifuata nakupigia kelele za mwizi.

Bodaboda: tobaa! Yamekuwa hayo tena. (Anawasha pikipiki yake na kuondoka.)

2. Kwa kutumia mifano, eleza dhana za kifasihi zifuatazo:

A. Visasili

B. Kituo bahari

C. Maghani

D. Muwala

E. Mkarara

Visasili ni hadithi ambazo hueleza kuhusu asili ya mambo fulani. Visasili husaidia kuelezea asili ya mambo yasiyoelezeka kama vile mauti, jando, tohara, ndoa na tamaduni/imani nyinginezo.

Kituo bahari ni msitari wa mwisho katika ubeti wa shairi ambayo hurudiwa katika kila ubeti.  Ni mstari unaotoka mwanzo hadi mwisho bila kubadilika katika kila ubeti.

Maghani ni tungo zinazotolewa kwa kughanwa (nusu kuimbwa nusu kukaririwa). Maghani yanaweza kuambatanishwa na ala za muziki au kughanwa kwa mdomo tu.

Muwala ni mtiririko wa mawazo ya malenga kutoka ubeti mmoja Hadi mwingine hasa kimaudhui. Yaani ukisoma unaelewa maelezo, hakuna kuchanganya.

Mkarara ni msitari wa mwisho katika ubeti wa wimbo au shairi ambao huimbwa kwa pamoja. Neno jingine la mkarara ni kiitikio, kibwagizo, kipokeo, takriri. Kwa mfano, wanafunzi waliitikia kwa sauti kwenye mkarara.

3. Kwa kutoa hoja tano, fafanua umuhimu wa nyimbo katika hadithi za fasihi simulizi.

Umuhimu wa nyimbo katika hadithi za fasihi simulizi

Kushirikisha hadhira.

Kubeba mafunzo mbalimbali. Kuelimisha.

Kuburudisha.

Kuhifadhi tamaduni za jamii.

Kukuza talanta na sanaa katika jamii.

4. Soma matini ifuatayo, kisha bainisha vipengele kumi vya lugha vilivyotumika.

Napenda mahala hapa kwa heba na utukufu wake, amani, ukimya, mkolezo wa ajabu na maumbile yake. Niko kwenye ufuko, nimekaa na gazeti langu li wazi. Sisikii, sioni, ingawa ninatarajia kwa apitaye mbali atadhani kuwa nimezama kwenye habari zilizokuwa kwenye gazeti; kumbe la hasha: nilivutiwa na uzuri wa madhari niliyoikabili kwenye mtiririko wa watoto warukao, wapigao mbio na kufukuzana kwenye pepo zipitazo, ziingiazo na zitokazo, kwenye bahari shwari isiyo na shari.

Vindege vionekanavyo vidogo vidogo, vijisamaki vidogo vidogo mashua na ngalawa ziyoyomazo, mbele zilizotia nanga na upepo mwanana unaotekenya hisia za mwili kwenye mazingira timamu kabisa, zilinipa raha ya dunia. Nikapigwa butwaa: nikaachama. Nikalia huku nimetabasamu. Nikalowa machozi ya furaha. Nikasema “Asiye na mwana aeleke jiwe.” nikapuliza ulizi, nikasawazika.

Kukaa hapa penye ufuko na kutembeza jicho langu kama dira huku nchi kavu na pale baharini kulinipa tajiriba si utani! Upeo wa macho, ule ambako mbingu ilionekana imeshikana na bahari. Mbingu ni bakuli lililofunika shani kubwa ya bahari.

Jua lilikuwa likizama. Na hapo ndipo utukufu wa mandhari haya unatimilika. Mtapanyikko wa rangi mbalimbali, zilizokaliana mchafukoge, zenye kutiwa nakshi na mvuto wa ajabu, nyekundu kwa athari, manjano inayochungulia kijivu, inayoshangilia bluu, imetamakani zambarau, imedokeza nyufa nyembamba za mistari ya fedha inayokoleza. Hakika mkono huu unajua kuchora. Nikajisemea moyoni Maulana! Jalali! Rabana!

Sarifu rangi zote unavyopenda. Sema milima na mabonde ya peponi ndivyo; sema konde ya mafuta ya makorongo sawa; sarifu vingine, tazama sasa yule mpiganaji, naye pia ana upanga wake yuko juu ya farasi akiakisi picha hii kwa jicho lake, ifuate; utaiona imekamilika sura hii hii haina hatima ya tafsiri, ndio maana waandishi na wachoraji wameandika na kuchora usanifu wa mwanadamu au maneno yaliyochorwa kwa ufasaha yanashindwa kukamilisha athari ya kuchwa kwa jua lile na athari ya mnaso wa sumaku; kwa wanaojua kutafsiri kwao wote ni miujiza.

Majibu

Vipengele vya lugha vilivyotumika ni:

- Takriri, mfano, “vidogovidogo.”

- Tashihisi, mfano, “upepo mwanana unaotekenya hisia za mwili.”

- Mjalizo, mfano, “Nikapigwa butwaa: nikaachama. Nikalia huku nimetabasamu.”

- Methali, mfano, “Asiye na mwana aeleke jiwe.”

- Sitiari, mfano, “Mbingu ni bakuli…”

- Nidaa, mfano, Nikajisemea moyoni Maulana! Jalali! Rabana!

- Ujenzi wa picha, mfano, “tazama sasa yule mpiganaji, naye pia ana upanga wake yuko juu ya farasi akiakisi picha hii kwa jicho lake, ifuate;”

- Ritifaa, mfano, “Nikajisemea moyoni Maulana! Jalali! Rabana!”

Pata Majibu ya Maswali yaliyobaki kwa Tsh. 1,000/= tu, Wasiliana na Mwalimu Hapa

Sehemu B (Alama 60)

Jibu maswali matatu kutoka sehemu hii. Swali la sita ni la lazima.

5. Tathilitha, tarbia na sabilia ni miundo katika ushairi. Kwa kutumia mifano dhahiri, bainisha jinsi miundo hiyo ilivyotumiwa na washairi katika diwani mbili ulizosoma.

6. Kwa kutumia diwani mbili ulizosoma, eleza wajibu unaotakiwa kwa viongozi ili kukidhi vilio vya watunzi wa mashairi. Toa hoja tatu kwa kila kitabu.

7. “Kuendelea kujadili nafasi ya mwanamke katika jamii ni upotevu wa rasilimali na muda.” Tathmini kauli hiyo kwa kutoa hoja nne zenye mifano kwa kila kitabu katika riwaya mbili ulizosoma.

8. Bainisha vipengele vya fasihi simulizi vilivyojitokeza katika tamthiliya mbili ulizosoma kwa kutoa hoja nne kwa kila tamthiliya.

Pata Majibu ya Maswali yaliyobaki kwa Tsh. 1,000/= tu, Wasiliana na Mwalimu Hapa

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2025