1. Kukosa hela ni vibaya sana, unaweza kukutana na ng’ombe ukahisi wanakusema. 2. Kama huna gari , huna nyumba, huna simu na huna hela, tofauti yako na kenge ni mkia. 3. Siyo kila anayeamka saa sita mchana ni tajiri, wengine wanapunguza saa za kuteseka. 4. Mtu mmoja aliota anaendesha gari, ikakwama kwenye matope, akaanza kuisukuma. Alipoamka, akajikuta yupo na kitanda jikoni. 5. Maisha ni ya ajabu sana, unakuta mtu hajaoa lakini chumba anachoishi kuna panya wana familia zao na yeye ndiyo anawalisha. 6. Ukiwa ugenini usinyamaze sana. Wenyeji wanaweza wakadhani unafikiria kuwaua. 7. Kila mtu anauogopa usiku. Kichaa mmoja alisikika akisema, “Usiku umeingia waniroge tena.” 8. Pombe mbaya, nimekutana na mlevi anatafuta wanawake wembamba atengeneze fagio. 9. Niliwahi kupanda basi, dereva analalamika njia nzima, “Nimefanya kazi miaka mingi, mafanikio hakuna. Sasa leo mwisho.” Abiria wakaanza kuomba kushuka mmojammoja. 10. Mchana hupati hela, usiku hupati usingizi. Kwa kifupi...